Skip to main content

WASICHANA 50 WAPEWA HAMASA YA MIL. 3 KUJIENDELEZA KIELIMU KASULU

Na Tryphone Odace, Kasulu - Kigoma.

WASICHANA 50 WAPEWA HAMASA YA MIL. 3 KUJIENDELEZA  KIELIMU KASULU

Na Tryphone Odace, Kasulu - Kigoma.

Taasisi ya Shukrani Foundation, imetoa vifaa vya Shule vyenye thamani ya Shilingi Milioni 3, kwa Wasichana 50 wa Msingi na Sekondari katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Mkoani Kigoma, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwahamasisha watoto wa kike kuhudhuria masomo na kuendelea na elimu.

Taasisi hiyo imekuwa ikitumia kauli mbiu ya “Nguvu ya Binti Ipo Kwenye Elimu”, inayolenga kuhamasisha na kusaidia watoto wa kike katika masuala mbalimbali, ikiwemo elimu na mahitaji muhimu yanayoweza kuwasaidia kufikia malengo yao.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Shukrani Foundation, Bi. Josephina Alphonce, ameeleza hatua zilizochukuliwa na taasisi hiyo katika kuwasaidia wanafunzi hao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Bogwe, Mwalimu David Kindanda, amewataka wazazi kuacha matumizi ya pombe kupita kiasi na badala yake kutumia rasilimali walizonazo kuhakikisha watoto wao wanapata mahitaji muhimu ya shule.

Amesema wazazi wana wajibu mkubwa katika kuhakikisha watoto wao wanapata mazingira bora ya kusoma na kufikia ndoto zao.

Akizungmza katika hafla hiyo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Kidyama, Amisa Juma Rajabu, amewataka wazazi kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto wao, pamoja na kujenga ukaribu nao ili waweze kuelewa changamoto zinazowakabili.

Amesisitiza kuwa wazazi wanapaswa kuwa karibu na watoto wao na kuwapa malezi yanayowawezesha kujenga ujasiri wa kuzungumza kuhusu changamoto wanazokutana nazo katika maisha na masomo.

Baadhi ya wazazi wa wasichana waliopatiwa vifaa hivyo wameishukuru Shukrani Foundation kwa msaada huo, wakisema vifaa hivyo vitawasaidia watoto wao katika masomo na kupunguza baadhi ya changamoto zinazoweza kuathiri mahudhurio yao shuleni.

Hatua hiyo ya Shukrani Foundation ni sehemu ya jitihada za taasisi hiyo katika kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu na kuwahamasisha kutambua kuwa elimu ni msingi muhimu wa kufikia ndoto na kujenga maisha bora ya baadaye.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.