Skip to main content

WASHIRIKI UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO KAGERA WAHIMIZWA UWAJIBIKAJI, MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA

Na Clavery Christian, Buukoba - Kagera.

WASHIRIKI UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO KAGERA WAHIMIZWA UWAJIBIKAJI, MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA

Na Clavery Christian, Buukoba - Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Ramadhani Kido, amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji kwa wadau wote wanaoshiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, akieleza kuwa matumizi sahihi ya fedha za umma ndiyo msingi wa mafanikio ya maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha iliyoandaliwa na TAKUKURU mkoani Kagera kuhusu usimamizi wa programu na miradi ya maendeleo, RC Kido amesema kila mdau anapaswa kutekeleza majukumu yake kwa weledi, uaminifu na kujituma ili kuhakikisha miradi inaleta matokeo chanya yaliyokusudiwa.

Alieleza kuwa ushirikiano na ufuatiliaji wa karibu wa miradi ni muhimu katika kuzuia changamoto zinazoweza kusababisha hasara kwa Serikali na kuchelewesha maendeleo.

Pia ameipongeza TAKUKURU kwa kuendelea kutoa elimu na kujenga uelewa kwa wadau mbalimbali kuhusu wajibu wao katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na kuwanufaisha wananchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.