Skip to main content

WARATIBU WAKUTANA KUIMARISHA AFUA ZA VVU, WASISITIZA USTAWI WA WATUMISHI MAHALA PA KAZI

Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Upendo Joseph Haule, amefungua mafunzo ya siku moja kwa Kamati za Uratibu wa Afua za VVU na UKIMWI, Magonjwa Yasiyoambukizwa na Waelimisha Rika kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri zote za mkoa wa Tabora, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi mjini Tabora.

WARATIBU WAKUTANA KUIMARISHA AFUA ZA VVU, WASISITIZA USTAWI WA WATUMISHI MAHALA PA KAZI
Studio Narration JAMBO FM

WARATIBU WAKUTANA KUIMARISHA AFUA ZA VVU, WASISITIZA USTAWI...

0:00 --:--

Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Upendo Joseph Haule, amefungua mafunzo ya siku moja kwa Kamati za Uratibu wa Afua za VVU na UKIMWI, Magonjwa Yasiyoambukizwa na Waelimisha Rika kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri zote za mkoa wa Tabora, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi mjini Tabora.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, kwa niaba ya katibu tawala mkoa wa Tabora, Bi. Haule amewataka viongozi na wasimamizi wa taasisi za Serikali kuhakikisha afua za VVU na UKIMWI zinajumuishwa katika mipango na bajeti za taasisi, huku akisisitiza umuhimu wa kulinda haki, utu na faragha za watumishi.

"Mtumishi mwenye afya ni msingi wa taasisi yenye tija; kulinda afya ya mtumishi ni kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi," amesema.

Aidha, amezitaka Kamati za Uratibu na Waelimisha Rika kuimarisha elimu kuhusu kinga dhidi ya VVU, upimaji wa hiari, huduma za matibabu na udhibiti wa magonjwa yasiyoambukizwa, sambamba na kupinga unyanyapaa na kuhakikisha taarifa za afya za watumishi zinatunzwa kwa usiri.

Awali, Afisa Utumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bi. Beatha Kumalija, amewahimiza watumishi kuzingatia lishe bora, mazoezi na kujiepusha na msongo wa mawazo na kuepuka unyanyapaa kazini.

Naye Dkt. Swaumu Kimaro kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete, amewasilisha mada kuhusu afya ya akili mahala pa kazi na namna ya kuhimili msongo na kuepuka mambo yanayoweza kusababisha athari kwa afya ya akili..

Katika majumuisho, wajumbe wamekubaliana kuimarisha utekelezaji wa afua za VVU, kutenga bajeti kwa wakati kwa ajili ya kuwasaidia watumishi wanaoishi na VVU kwa kuzingatia usiri na taratibu husika, pamoja na kuanzisha bonanza za michezo kwa ajili ya kuimarisha afya na mshikamano wa watumishi.

Pia wamesisitiza kupewa kipaumbele kwa ajenda ya afya ya akili na kinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.