Skip to main content

WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA KUPATA AHUENI

Na Eunice Kanumba -Shinyanga.

WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA KUPATA AHUENI

Na Eunice Kanumba -Shinyanga.

Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi za kwanza Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuanzisha huduma za utoaji wa dawa  kwa waraibu wa dawa za kulevya (MENTHADONE) ambapo hadi  sasa, kuna vituo kadhaa vinavyotoa huduma hizi, vikihudumia maelfu ya waraibu na kusaidia wengi kurejea katika maisha ya kawaida .

Miongoni mwa mikoa iliyoanzisha kituo hicho  (KILINIKI)  ni mkoa wa Shinyanga ambapo kiliniki hiyo imejengwa  kwa msaada wa shirika la Tanzania health promotion support (THPS) benki ya CRDB kwa tahamni ya shilingi milioni 145  na kuikabidhi  rasimi  kwa serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia manispaa ya Shinyanga  hatua ambayo inalenga kuimarisha  juhudi za mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Kukamilika kwa kiliniki hiyo mkoani Shinyanga ni matokeo ya mashirikiano mazuri kati ya wadau hao pamoja na wizara ya afya DCEA na ofisi ya waziri mkuu-TAMISEMI kwa kuzingatia viwango vya kitaifa vya huduma ya afya  

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo.

Akizungumzia uanzishwaji wa kituo hicho katika mkoa wa Shinyanga   Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amesema kuwa kliniki hiyo ni nyenzo muhimu katika kupunguza madhara ya uraibu wa dawa za kulevya.

Amesema uanzishwaji wa kituo hicho kutapelekea jamii katika mkoa huo kuwa salama  kwani waraibu wengi hujikuta wakijihusisha na vitendo vya uahalifu ili kupata fedha za kununua dawa za kulevya hivyo watakapoanza kupata matibabu ya menthadonekuatondoa utegemezi huo pamoja na uhalifu.

DCEA Lyimo amesema kiliniki hiyo pia inakwenda  Kurejesha Nguvu Kazi ya taifa kwani waraibu wote watapata matibabu na kurejea makazini na kuchangia katika maendeleo ya uchumi na kwamba jamii inapaswa kuelewa kuwa uraibu ni tatizo la kiafya linaloweza kutibika hivyo jamii haina budi kukitumia kituo hicho.

Muonekano wa

Aidha, amewapongeza wadau waliofanikisha ujenzi huo, likiwemo Shirika la THPS na Benki ya CRDB, akieleza kuwa mchango wa sekta binafsi unaonyesha namna taasisi za kifedha zinavyoweza kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto za kijamii.

“Napenda kuipongeza na kuishukuru THPS kwa jitihada zao za kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya. Pia naishukuru Benki ya CRDB kwa msaada wao mkubwa. Nawahimiza wananchi, hususan vijana walioathirika, kutumia huduma hizi ili kwa pamoja tulinde afya na mustakabali wa jamii zetu,” amesema Lyimo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia, amesema kabla ya kuanzishwa kwa kliniki hiyo, waraibu wengi wa dawa za kulevya kutoka Shinyanga walilazimika kusafiri hadi Mkoa wa Mwanza kupata matibabu, hali iliyosababisha baadhi yao kushindwa kufikia huduma hizo kwa urahisi.

Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia.

Dkt. Redempta ameeleza kuwa ndipo walipoamua kuomba ufadhili kutoka CRDB Bank ili kujenga kituo hicho, ambacho sasa ni cha kwanza cha aina yake katika Mkoa wa Shinyanga.

“Tunajivunia kuona jitihada hii muhimu ikifanikiwa. Naishukuru Benki ya CRDB kwa msaada wao na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wake endelevu. Huu ni mfano mzuri wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi katika kuimarisha upatikanaji, usawa na ubora wa huduma za afya, sambamba na ajenda ya Uhakika wa Afya kwa Wote,” amesema Dkt. Redempta.

Naye meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid M. Nsekela, amesema benki hiyo ina utaratibu wa kutenga asilimia moja ya faida baada ya kodi (VAT) kwa ajili ya kurejesha kwa jamii kupitia miradi ya afya, elimu, mazingira na maeneo mengine ya kijamii.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Nsekela.

“Huu ni mwendelezo na tunaahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kusaidia miradi ya serikali. Tunaamini katika mashirikiano ya Serikali na sekta binafsi ndo chachu ya mafanikio katika maendeleo. ”,ameongeza Wagana.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, amesema tayari maandalizi muhimu yamekamilika ikiwemo upatikanaji wa watumishi wa afya, samani za kliniki pamoja na maboresho ya mazingira ya kituo hicho ili kuhakikisha huduma zinaanza kutolewa kwa ufanisi.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile.

Aidha, ameomba wadau kuendelea kuunga mkono kituo hicho kwa kukiwezesha kupata vifaa muhimu zaidi ikiwemo mashine za kupima kiwango cha matumizi ya dawa (meter measure) ili kusaidia kupanga dozi sahihi kwa wagonjwa kulingana na kiwango cha uathirika.

Uanzishwaji wa kituo cha menthadone (kiliniki) mkoani humo hatua inayolenga  kurejesha utu wa binadamu, na kujenga jamii yenye afya na maendeleo, Ushirikiano kati ya serikali, wataalamu wa afya, na jamii kwa ujumla ni msingi wa kuhakikisha mafanikio  na kuokoa kundi kubwa la vijana ambalo kwa asilimia kubwa limejiingiza katika janga la uraibu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.