Skip to main content

WAOMBA MCHAKATO MALIPO KABLA HUDUMA BILI ZA MAJI UHARAKISHWE, SHUWASA YATOA HAKIKISHO

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

WAOMBA  MCHAKATO  MALIPO KABLA HUDUMA BILI ZA MAJI UHARAKISHWE, SHUWASA YATOA HAKIKISHO

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Wananchi wa Manispaa ya Shinyanga wamiomba mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) kuharakisha mchakato wa kuanza kutumia mita za malipo ya kabla ili kuondoa malalamiko yanayoendelea kwamba wasomaji wa mita za maji wamekuwa na tabia ya kuwabambikia bili kubwa za maji pindi wanapopita kusoma.

Wananchi hao wameyasema hayo katika  mkutano wa wadau wa maji ulioketi kujadili  rasimu ya mkataba mpya ya huduma kwa wateja, ambapo pia wamepongeza kai nzuri inayofanywa na mamlaka hiyo ya kuhudumia wananchi kwani kwa sasa pamekuwa hakuna tatizo la kukatika maji pasipo taarifa kama ilivyokuwa awali.

Mkurugenzi wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa Mtaa wa Viwandani Manispaa ya Shinyanga, Ashraf Said amesema pamoja na maboresho ya huduma ya maji, changamoto ya bili kubwa bado inaumiza wananchi wengi.

“Tunawaomba SHUWASA muendelee kutoa huduma bora kwa wateja wenu, lakini ili kuondoa malalamiko ya bili kubwa za maji, tuwekeeni mita za malipo ya kabla kama ilivyo kwenye umeme wa ruku, tokeni zikiisha maji yanakata,” amesema Ashirafu.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja SHUWASA, Rueben Mwandumbya.

Naye Mgeni rasmi katika kikao cha kujadili rasimu hiyo  Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro amewataka SHUWASA kutoa  kwa kuzingatia  mkataba wa huduma kwa wateja na miongozi ya kisheria, ikiwa ni pamoja na   kutoa huduma bora ya maji kwa wananchi na kushughulikia matatizo au kero zao kwa wakati.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola, amesema mipango ya kuanza kutumia mita za malipo ya kabla ipo, lakini utekelezaji wake utafanyika kwa awamu kutokana na gharama kubwa za vifaa hivyo.

Wananchi wanaiomba SHUWASA kuharakisha mchakato wa kuanza kutumia mita za malipo ya kabla.

Amefafanua kuwa hatua ya mwanzo itahusisha maeneo yenye changamoto kubwa za ulipaji, hususan vituo vya umma vya maji, huku zoezi hilo likitarajiwa kuanza Aprili mwaka huu.

Amesema ufungaji  wa mita za malipo ya kabla, utafanyika kwa hatua sababu zina gharama kubwa ikilinganishwa na mita za kawaida, na kwamba mita hizo wataanza kuzifunga kwanza kwenye maeneo ambayo yanachangamoto za ulipaji bili za maji hasa kwenye vituo vya umma vya kuchotea maji na zoezi hilo wanatarajia kuzifunga mwenzi Aprili 2026.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Salum Kitumbo.

Akizungumzia rasimu ya mkataba wa huduma kwa wateja  Mhandisi  Katopola, amesema mkataba wa huduma kwa wateja uliokuwepo umeisha, na sasa wapo kwenye kujadili rasimu ya mkataba mwingine ambao utadumu kwa muda wa miaka mitatu kuanzia 2026 hadi 2029 na utatumika mara baada ya kupitishwa na Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji. EWURA.

Amesema mkataba huo una umuhimu mkubwa, kwa kuwa unaweka bayana haki na wajibu wa pande zote mbili, mtoa huduma na mteja, kwa lengo la kuongeza uwazi, uwajibikaji na kujenga uhusiano imara.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro.

Naye Mkurugenzi wa huduma kwa wateja kutoka SHUWASA, Rueben Mwandumbya akiwasilisha wasilisho la mkataba wa huduma kwa wateja, ametaja majukumu ya mamlaka hiyo kwa wateja, kuwa ni kutoa huduma ya majisafi na salama yanayotosheleza katika viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa, kutoa huduma ya usafi wa mazingira .

Wadau wa Maji.

Wajibu mwingine ni kulinda na kutunza mali na vyanzo vya maji, kutoa elimu kwa wateja juu ya sera ya taifa ya maji, kuwahamasisha wateja kulipa ankra za maji za kila mwezi kwa wakati na kulipa madeni ya maji, kupokea na kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto au malalamiko ya wateja, kukagua na kudhibiti uvujaji wa maji na kutunza kumbukumbu za wateja.

Wajibu wa Mteja kwa Mamlaka ni pamoja na kulipa ankara za Maji kwa wakati.

Ameongeza, pia kutoa maendeleo ya uendeshaji wa shughuli za mamlaka kwa wateja na umma kwa ujumla, kupendekeza bei za utoaji wa huduma za majisafi na majitaka kulingana na gharama za uendeshaji na kwa kuzingatia hali ya uchumi wa wateja, kumshirikisha mteja pindi zoezi la usomaji wa dira linapofanyika ili aweze kujua matumizi yake.

Mwandumbya pia ameanisha haki za mamlaka ya SHUWASA kwa wananchi kuwa ni ni kulipwa ankra za huduma ya majisafi na usafi wa mazingira, kulipwa malipo halali kutokana na huduma inayotolewa kwa mteja, kusitisha huduma ya maji kwa mteja asiyelipa kwa wakati ankra za maji ndani ya siku 30, kuchukua hatua za kisheria kwa waharibifu wa miundombinu pamoja na wezi wa maji.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Viwandani Manispaa ya Shinyanga, Ashraf Said.

Pia ameweka wazi kuhusu wajibu wa mteja kwa mamlaka kuwa ni pamoja na Kulipa ankra za maji kwa wakati, kutoa ushirikiano kwa watumishi wa mamlaka wanapowahudumia, kutoa taarifa sahihi za rushwa, wizi wa maji na uharibifu wa mali za mamlaka, kulinda na kutunza vyanzo vya maji, na kuhudhuria mikutano inayoitishwa na mamlaka ili kupata taarifa mbalimbali.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.