Skip to main content

WANUFAIKA MIKOPO YA ASILIMIA 10 WAPEWA NENO IGUNGA

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Shabani Hemed, ameishukuru Serikali ya kwa kuendelea kuwawezesha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kupitia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya halmashauri.

WANUFAIKA MIKOPO YA ASILIMIA 10 WAPEWA NENO IGUNGA

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Shabani Hemed, ameishukuru Serikali ya kwa kuendelea kuwawezesha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kupitia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya halmashauri. 

Amezungumza hayo wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo kwa vikundi 47 vilivyokidhi vigezo katika ukumbi wa Maxwel mjini Igunga, huku akisema hatua hiyo itasaidia kuongeza fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa.

Aidha, amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia kwa shughuli za maendeleo kama walivyoomba na kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya fedha huku akisisitiza kuwa faida inayopatikana kutokana na biashara ndiyo itumike kukidhi mahitaji mbalimbali huku mtaji ukiendelea kuimarishwa.

Katika hatua nyingine, Hemed alisema Halmashauri ya Wilaya ya Igunga inatarajia kujitegemea zaidi katika utekelezaji wa bajeti yake ya maendeleo, akibainisha kuwa asilimia 74.2 ya bajeti ya maendeleo kwa mwaka ujao itatokana na mapato ya ndani badala ya kutegemea wahisani ambapo meeleza kuwa fedha hizo zitatumika kuboresha barabara, kuchimba visima na kuimarisha upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Basu Masumbuko, amewahimiza vijana kutafuta taarifa sahihi ili kufanya maamuzi yenye manufaa na kuepuka upotoshaji unaosambazwa kupitia mitandao ya kijamii.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Bi. Selwa Hamid, amevitia moyo vikundi vilivyokosa mikopo katika awamu hii kuwa na subira kwani utoaji wa mikopo utaendelea katika awamu zijazo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.