Skip to main content

WANNE WAKAMATWA TUHUMA ZA KUPIGA MABASI MAWE SINGIDA

Na Saulo Stephen – Singida.

WANNE WAKAMATWA TUHUMA ZA KUPIGA MABASI MAWE SINGIDA

Na Saulo Stephen – Singida.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SACP Amon Kakwale amesema Jeshi la Polisi mkoani humo limewakamata watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kupiga mawe mabasi mbalimbali yanayopita katika barabara kuu za Mkoa wa Singida, matukio yaliyosababisha uharibifu wa vioo vya magari hayo.

SACP Kakwale ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake, akieleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo tofauti kati ya Mei 21 hadi Mei 24, 2026 kufuatia operesheni za kuzuia na kutanzua uhalifu zilizofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi.

Amesema mtuhumiwa wa kwanza ni Juma Zuberi Bahali (35) mkazi wa Ikungi ambaye alikamatwa kwa tuhuma za kupiga mawe na kuvunja kioo cha basi la kampuni ya SATCO lililokuwa likitokea Bukoba kuelekea Dodoma katika eneo la Issuna Wilaya ya Ikungi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP Amon Kakwale.

Aidha amesema watuhumiwa wengine wawili ambao ni Aidan Jumanne Kitwana (21) na Ramadhani Juma Mgesi (23), wakazi wa Ulyampiti Wilaya ya Ikungi, walikamatwa Mei 23, 2026 kwa tuhuma za kupiga mawe basi la kampuni ya KATARAMA lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Dodoma na kusababisha kuvunjika kwa kioo cha basi hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda Kakwale, mtuhumiwa wa nne ni Jacobo Petro Musa (29) mkazi wa Njiri Wilaya ya Manyoni ambaye alikamatwa Mei 24, 2026 kwa kosa la kupiga mawe basi lingine la kampuni ya KATARAMA lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Dar es Salaam na kuharibu ubavuni wa kioo cha gari hilo.

SACP Kakwale amewatahadharisha wananchi kuacha vitendo vya uharibifu wa mali na uvunjifu wa sheria, akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya watu wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya kihalifu mkoani Singida.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.