Skip to main content

WANASIASA WATAKAOKUTANA NA KABILA KUCHUKULIWA HATUA - SERIKALI DRC

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imetishia kuwachukulia hatua wanasiasa wataokwenda Goma kukutana na rais mstaafu Joseph Kabila.

WANASIASA WATAKAOKUTANA NA KABILA KUCHUKULIWA HATUA - SERIKALI DRC

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imetishia kuwachukulia hatua wanasiasa wataokwenda Goma kukutana na rais mstaafu Joseph Kabila.

Kauli hiyo, imetolewa na Naibu Waziri Mkuu wa Mambo ya Ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jacquemin Shabani, baada ya muungano wa C64 kuanzisha mchakato wa kukutana na rais, Felix Tshisekedi na mstaafu Joseph Kabila.

Muungano wa vyama vya kisiasa nchini DRC (C64), unaopinga marekebisho ya katiba, hivi karibuni walikutana Roma Italia, kutathmini harakati za kisiasa za kupinga marekebisho ya katiba na kuwa na msimamo mmoja baada ya rais wa zamani Joseph Kabila kutangaza kuongoza kundi la FRN.

Kufuatia tangazo hilo, Naibu Waziri Mkuu wa Mambo ya Ndani Jacquemin Shabani, amesema hakuna mtu anayeweza kuwasiliana na adui katika eneo linalokaliwa bila idhini ya serikali.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.