Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amewataka wote wanaomiliki na kutumia silaha kujitokeza katika mamlaka husika, ili zifanyiwe ukaguzi, huku akiwataka wamiliki wa mabasi yasiyo na vibali vya kuegesha Shekilango kuhamishia shughuli zao Kituo cha Magufuli ndani ya siku saba.
RC Chalamila ameyasema hayo hii leo Agosti 11, 2026 ambapo pia amewataka Watu wanaomiliki au kutumia silaha bila vibali halali kujisalimisha mara moja kwa mamlaka husika, ikiwa ni sehemu ya hatua za kudhibiti matukio ya wizi na uhalifu katika Mkoa wa Dar es salaam.

Amesema, "kuanzia tarehe ya leo mpaka kufikia tarehe 17 yani siku ya jumatatu wale wote ambao hawana vibali vya kuoperate stendi zao katikati ya Mji warudishe mabasi yao Stendi ya Magufuli."
Discussion
Reader comments
0 contributions