Skip to main content

WANAODAIWA KUGHUSHI NYARAKA KUJIPATIA MKOPO HESLB WAFIKISHWA MAHAKAMANI, BODI YAONYA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imewaonya waombaji wa mikopo kuacha vitendo vya kughushi nyaraka kwa lengo la kujipatia mikopo isivyo halali.

WANAODAIWA KUGHUSHI NYARAKA KUJIPATIA MKOPO HESLB WAFIKISHWA MAHAKAMANI, BODI YAONYA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imewaonya waombaji wa mikopo kuacha vitendo vya kughushi nyaraka kwa lengo la kujipatia mikopo isivyo halali.

Onyo hilo limetolewa kufuatia Wanafunzi 17 pamoja na mhitimu mmoja kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya juu jijini Dar es Salaam, kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka ya kughushi nyaraka, kutoa taarifa za uongo na kujipatia mikopo kwa udanganyifu.

Washitakiwa hao ni kutoka katika vyuo vya IFM, CBE, UDSM, NIT, DMI, MNMA, DIT na Chuo Kikuu cha Kairuki, ambao wanadaiwa kughushi nyaraka wakionesha kuwa Baba zao ni Watu wenye Ulemavu, ili kujipatia mikopo isivyo halali.

Mahakama imeelezwa kuwa kati ya Juni 2024 na Novemba 2025, washitakiwa hao walitumia mfumo wa OLAMS kuwasilisha taarifa za uongo, ikiwemo madai ya ulemavu wao au wa wazazi wao ili kupata kipaumbele katika mikopo ya elimu ya juu.

Baadhi yao wanadaiwa kufanikiwa kupata mikopo yenye thamani ya mamilioni ya shilingi kupitia mbinu hizo, Ikidaiwa kuwa makosa hayo yalitendeka mwaka 2025 kupitia mfumo wa mtandao wa maombi ya mikopo wa OLAMS (Online Loan Application and Management System).

Washtakiwa hao ni pamoja na Frank Kayamba, Sophia Macha, Clara Nyarusai, Eline Urio, Brian Assem, Loveness Mrutu, Elias Kasiga, Eva Namjuzi, Silass Silass, Nyasilu Magadula, Badru Lenga, Aziza Bashiru, Anitha Godfrey, Cyprian Champunga, Elneth Nyagawa, Idrisa Omary, Mohamedi Mohamedi na Michael Shoide.

Hata hivyo, Washtakiwa wote wako nje kwa dhamana kufuatia kujidhamini wenyewe kwa vitambulisho vyao na kesi imeahirishwa hadi Juni 9, 2026 kwa ajili ya hatua za awali baada ya upelelezi kukamilika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.