Skip to main content

WANAOBADILI MATUMIZI YA VYANDARUA MARA WAONYWA

Na Adam Msafiri - Mara.

WANAOBADILI MATUMIZI YA VYANDARUA MARA WAONYWA

Na Adam Msafiri - Mara.

Serikali mkoani Mara imewaonya wananchi dhidi ya kubadili matumizi ya vyandarua vitakavyogawiwa katika kampeni ya kitaifa ya kudhibiti malaria, ikiwemo kuvitumia kuvulia samaki, kufugia kuku au kwa matumizi mengine yasiyokusudiwa.

Onyo hilo limetolewa wakati Mkoa wa Mara ukijiandaa kuanza zoezi la ugawaji wa vyandarua zaidi ya milioni moja vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 22, litakalofanyika kuanzia Agosti 10 hadi 20, 2026 katika halmashauri zote za mkoa huo.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya kampeni hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amesema serikali haitamvumilia mtu yeyote atakayebainika kutumia vyandarua hivyo kinyume na lengo lake la kuzuia maambukizi ya malaria.

Mtambi ameagiza mamlaka husika kuchukua hatua kali za kisheria⁷ dhidi ya watakaokiuka maelekezo hayo ili kuhakikisha rasilimali iliyowekezwa na serikali inaleta matokeo yaliyokusudiwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Kwa upande wake, Mratibu wa Kampeni ya Taifa ya Ugawaji Vyandarua kutoka Wizara ya Afya, Wilfred Mwafongo, amesema Mkoa wa Mara umepewa kipaumbele kutokana na kuwa wa pili nchini kwa maambukizi ya malaria baada ya Mkoa wa Kagera.

Amesema kampeni hiyo inalenga kuongeza matumizi sahihi ya vyandarua kwa wananchi wote walio katika maeneo yenye maambukizi makubwa, hatua inayotarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa visa vya malaria.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dkt. Stanley Kajuna, amewataka wananchi kutotegemea matumizi ya vyandarua pekee, bali pia kuendelea kuharibu mazalia ya mbu kwa kusafisha mazingira yanayozunguka makazi yao.

Amesema shughuli mbalimbali za kiuchumi zimekuwa zikichangia kuwepo kwa maji yaliyotuama, ambayo ni mazalia ya mbu wanaosababisha malaria, hivyo ushiriki wa jamii katika usafi wa mazingira ni muhimu.

Kwa upande wake, Dkt. Ruth Msolla kutoka Mradi wa PMI amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, wadau wa maendeleo na wananchi katika kuhakikisha vyandarua vinatumika ipasavyo ili kufikia malengo ya kupunguza maambukizi ya malaria.

Serikali ina matumaini kuwa kupitia kampeni hiyo pamoja na utekelezaji wa mikakati mingine ya kudhibiti malaria, Mkoa wa Mara utaweza kufikia lengo la kutokuwa na visa vya malaria ifikapo mwaka 2030.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.