Na Afarah Suleiman, Kiteto - Manyara.
Wananchi zaidi ya 25,000 Wilayani Kiteto Mkoani Manyara wameanza kunufaika na mradi mpya wa maji safi na salama, unaotekelezwa na Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).
Wananchi hao ni kutoka vijiji vinne vya Engusero, Ngupa, Nasentan na Nchimila vya Wilayani humo, ambapo Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara, Mhandisi Jemes Kionaomela akitoa taarifa kwa Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael amesema, mradi huo umegharimu Shilingi Bilioni 1.6 na umefikia asilimia 74.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo, Wazo ameipongeza RUWASA kwa kutekeleza mradi huo wenye ubora na kusisitiza wananchi umuhimu wa kutunza miundombinu ya maji, ili iwe endelevu.
Nao baadhi ya wananchi wa walionufaika na mradi huo katika kijiji cha Nchinila, wameishukuru Serikali kwa utekelezaji huo na kusema utawaondolea adha waliyokuwa nayo ya kufuata maji umbali mrefu na kushindwa kufanya shughuli za maendeleo kwa wakati.







Discussion
Reader comments
0 contributions