Skip to main content

WANANCHI, WATUMISHI WA AFYA SINGIDA WAJIPANGA KUBORESHA MAZINGIRA ZAHANATI ITITI

Wananchi wa Kata ya Uhamaka kwa kushirikiana na watumishi wa Idara ya Afya wameonyesha mshikamano kwa kuchangishana na kutekeleza mradi wa kuboresha mazingira katika Zahanati ya Ititi, Manispaa ya Singida.

WANANCHI, WATUMISHI WA AFYA SINGIDA WAJIPANGA KUBORESHA MAZINGIRA ZAHANATI  ITITI
Studio Narration JAMBO FM

WANANCHI, WATUMISHI WA AFYA SINGIDA WAJIPANGA KUBORESHA MAZI...

0:00 --:--

Wananchi wa Kata ya Uhamaka kwa kushirikiana na watumishi wa Idara ya Afya wameonyesha mshikamano kwa kuchangishana na kutekeleza mradi wa kuboresha mazingira katika Zahanati ya Ititi, Manispaa ya Singida.

Mradi huo unalenga kuboresha mazingira ya zahanati hiyo na kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa, watumishi wa afya pamoja na wananchi wanaofika kupata huduma.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika katika Zahanati ya Ititi, Naibu Meya wa Manispaa ya Singida, Abdallah Mkoko, kwa niaba ya Meya wa Manispaa ya Singida, Geoffrey Mdama, aliwapongeza wananchi na wadau wote walioshiriki katika kufanikisha mradi huo.

Mkoko amesema hatua hiyo ni mfano wa namna wananchi wanavyoweza kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma za kijamii, hususan sekta ya afya.“Leo tumeona nguvu ya wananchi. Kata ya Uhamaka mmeunga mkono Mtaa wa Ititi na mmeonyesha kuwa afya ya jamii ni jukumu letu sote.

Manispaa ya Singida itaendelea kuwashika mkono,” alisema Mhe. Mkoko.Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Ititi, Dkt. Aminiel Elisamson, amesema maboresho hayo yatachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa katika kituo hicho.

Amesema mazingira safi na bora ni sehemu muhimu ya huduma za afya, huku akiwashukuru wananchi, watumishi na wadau wote walioshiriki kwa namna mbalimbali katika kufanikisha mradi huo.

Zahanati ya Ititi ilianza kutoa huduma rasmi Septemba 2023 na imekuwa ikihudumia wananchi kutoka ndani na nje ya Kata ya Uhamaka.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.