Skip to main content

WANANCHI WATOA SHUKRAN KUREJEA KWA MAWASILIANO YA BARABARA KIUNGANISHI GEITA-KAHAMA

Na Ibrahim Rojala - Geita.

WANANCHI WATOA SHUKRAN KUREJEA KWA MAWASILIANO YA BARABARA KIUNGANISHI GEITA-KAHAMA

Na Ibrahim Rojala - Geita.

Wananchi wa vijiji vya Buyagu na Nyalazwaja, vilivyopo katika kata za Nyakamwaga na Nyalazwaja, Wilaya ya Geita, wameishukuru Serikali kwa kutatua changamoto ya muda mrefu ya usafiri na mawasiliano kupitia ujenzi wa daraja linalounganisha vijiji hivyo na kurahisisha usafiri kutoka Geita kuelekea Wilaya ya Kahama.

Akitoa taarifa kwa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Geita wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Geita, Mhandisi Cathbert Paul, amesema mradi huo ulianza kutekelezwa tarehe 28 Machi 2026 na unatarajiwa kukamilika tarehe 25 Novemba 2026.

Amesema ujenzi wa daraja hilo unagharimu jumla ya shilingi milioni 590 na unalenga kuboresha miundombinu ya usafiri, kurahisisha shughuli za kiuchumi na kuongeza huduma za kijamii kwa wananchi wa maeneo hayo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashimu Komba, ameihakikishia Kamati ya Siasa ya CCM kuwa ataendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo ili ikamilike kwa wakati na kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita, Barnabas Mapande, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutatua changamoto za wananchi kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa daraja hilo ambalo litachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo husika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.