- Na Afarah Suleiman, Hanang' - Manyara.
Naibu Waziri wa Maji, Kundo Mathew, amewahakikishia Wananchi wa Wilaya ya Hanang’ kuwa Serikali itaendelea kuwapatia huduma ya maji safi na salama katika vijiji vyote ambavyo bado havijafikiwa na huduma hiyo.
Kundo amesema hayo akiwa Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, wakati akiendelea na ziara yake ya siku mbili mkoani humo, ambapo amemuagiza Meneja wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini RUWASA Mkoa wa Manyara, kuhakikisha wananchi hawatembei zaidi ya kilomita mbili kufuata huduma ya maji, kwa kuwasogezea huduma hiyo karibu na makazi yao. 
Awali, Mbunge wa Jimbo la Hanang’, Asia Halamgha, amemuomba Naibu Waziri wa Maji kuhakikisha fedha zinapelekwa wilayani humo kwa ajili ya kuchimba visima katika maeneo ambayo hayana huduma ya maji, ili wananchi waweze kunufaika na huduma hiyo.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ amesema maelekezo yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Maji yatatekelezwa kwa wakati, huku akisisitiza ushirikiano wa wananchi katika kulinda na kutunza miundombinu hiyo ya maji.

MWISHO.
Discussion
Reader comments
0 contributions