Skip to main content

WANANCHI SABURI WAIOMBA SERIKALI KUZUIA UBOMOAJI WA NYUMBA ZAIDI YA 600

Wananchi wa Kitongoji cha Saburi, kilichopo Kata ya Makuyuni, wameiomba Serikali kuingilia kati kwa haraka ili kuzuia kile walichodai kuwa ni jaribio la kubomoa zaidi ya nyumba 600 pamoja na taasisi za kijamii zilizopo katika eneo hilo.

WANANCHI SABURI WAIOMBA SERIKALI KUZUIA UBOMOAJI WA NYUMBA ZAIDI YA 600
Studio Narration JAMBO FM

WANANCHI SABURI WAIOMBA SERIKALI KUZUIA UBOMOAJI WA NYUMBA Z...

0:00 --:--

Wananchi wa Kitongoji cha Saburi, kilichopo Kata ya Makuyuni, wameiomba Serikali kuingilia kati kwa haraka ili kuzuia kile walichodai kuwa ni jaribio la kubomoa zaidi ya nyumba 600 pamoja na taasisi za kijamii zilizopo katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa niaba ya wananchi hao, wamesema wameishi katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 30, ambapo awali walidai walikabidhiwa maeneo hayo kihalali na mwekezaji aliyekuwepo kabla, kabla ya Halmashauri kuyapima na kuweka alama za mipaka.

Wamesema, eneo hilo kwa sasa linatambulika kama Kitongoji kinachojitegemea na lina shule, zahanati, misikiti, kanisa, umeme wa REA na visima vya maji.

Wananchi hao, pia wamedai kuwa mwaka 2025 Halmashauri ilimuandikia mwekezaji Akram Aziz barua ya kumtaka kuachia eneo lenye ukubwa wa ekari 400 kwa ajili ya kupisha makazi ya wananchi, lakini madai yao ni kwamba agizo hilo halikutekelezwa.

Wamesema, hatua hiyo imeendelea kuwa chanzo cha mvutano kuhusu umiliki na matumizi ya ardhi katika eneo hilo.

Katika tukio walilolitaja kuwa ni la Oktoba 2, 2026, wananchi hao wamedai mwekezaji huyo alifika katika Kitongoji cha Saburi akiwa na tingatinga kwa lengo la kuanza kubomoa nyumba pamoja na baadhi ya taasisi za kijamii.

Wamesema, tukio hilo lilisababisha taharuki na vurugu kati ya wananchi na watu waliodaiwa kuambatana na mwekezaji, hali iliyosababisha upande huo kuondoka eneo hilo.

Kutokana na hali hiyo, wananchi hao wameziomba Ofisi za Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa kuchukua hatua za dharura kwa kumzuia mwekezaji huyo kufanya ubomoaji, kuchunguza hati na nyaraka zinazotumika katika madai ya umiliki wa eneo hilo, pamoja na kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao.

Wamesema hatua hizo ni muhimu, ili kulinda amani na kuzuia uwezekano wa kuibuka kwa vurugu zaidi katika eneo hilo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.