Skip to main content

WANANCHI NGAGANULWA KUFIKIWA NA MAJI YA ZIWA VICTORIA

WANANCHI WA NGAGANULWA KUFIKIWA NA MAJI YA ZIWA VICTORIA

WANANCHI NGAGANULWA KUFIKIWA NA MAJI YA ZIWA VICTORIA
Studio Narration JAMBO FM

WANANCHI NGAGANULWA KUFIKIWA NA MAJI YA ZIWA VICTORIA

0:00 --:--

WANANCHI WA NGAGANULWA KUFIKIWA NA MAJI YA ZIWA VICTORIA

Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, amesema wananchi wa Kijiji cha Ngaganulwa Kata ya Usanda wilayani Shinyanga, hivi karibuni wataondokana na adha ya ukosefu wa maji, baada ya yeye kuzungumzia bungeni changamoto hiyo ya ukosefu wa maji, na kisha serikali kuanza kutoa fedha kwa ajili ya usambazaji wa maji kutoka Ziwa Victoria.

MBUNGE WA JIMBO LA ITWANGI AZZA HILAL

AzzaAmebainisha hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji hicho katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru, pamoja na kusikiliza kero zao na kuzitolea majibu.

Amesema, maji hayo yatatoka katika Tenki la Buchama, ambayo yatapita kijiji cha Jomu, na kisha kufika kijiji hicho cha Ngaganulwa hadi Usanda.

“Awamu ya kwanza katika Kijiji cha Ngaganulwa vitawekwa vituo vya kuchotea maji, ili wananchi muanze kutumia hayo maji. Baada ya hapo, awamu ya pili mtaruhusiwa sasa kila mwenye uwezo wa kuvuta maji nyumbani kwake avute,” amesema Azza.

Katika hatua nyingine, amewapongeza wananchi wa kijiji hicho kwa kuanzisha ujenzi wa zahanati kwa nguvu zao wenyewe, na kufikia hatua ya renta pamoja na kuweka jamvi, huku akiwaunga mkono kwa kuwapatia fedha Sh. 405,000 ambazo wanadaiwa katika ujenzi huo na kuhaidi kuwa katika bajeti zake mwakani ataweka pia zahanati hiyo ili iweze kupauliwa.

Naye Meneja wa RUWASA wilayani Shinyanga, Mhandisi Emmael Nkopi, akizungumza kwa njia ya simu kwenye mkutano huo, amesema baada ya maagizo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, walitembelea maeneo ya Itwangi, ikiwamo Kata ya Usanda, na tayari wamefanya usanifu.

Amesema watatoa maji katika Tenki la Buchama, na tayari wamepewa kibali cha kupeleka maji Kijiji cha Singita na kufika Kijiji cha Ngaganulwa, kwa sababu kipo njiani kuelekea Singita, huku akibainisha kuwa, tayari wametangaza ununuzi wa mabomba.

Changamoto nyingine zilizozungumziwa kwenye mkutano huo ni pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara, na ukosefu wa umeme katika ngazi ya vitongoji.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.