Wananchi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara, wameonywa kuacha mara moja uvamizi wa maeneo ya hifadhi ya misitu, huku Serikali ikianza oparesheni maalumu ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaochangiwa na ukataji miti na shughuli za kibinadamu.
Onyo hilo limetolewa Machi 20,2026 na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka wakati wa zoezi la upandaji miti kuelekea maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani, ambapo amesisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuvamia maeneo yaliyohifadhiwa.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya ameagiza viongozi wa serikali za mitaa kusimamia kikamilifu sheria ndogo katika maeneo yote yaliyopandwa miti, huku baadhi ya wananchi wakionesha kuunga mkono juhudi hizo wakidai uharibifu wa mazingira unaathiri moja kwa moja maisha yao.

Kwa upande wake, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wilayani Musoma, umesema tayari umepanda miti zaidi ya elfu mbili na mia tano ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kurejesha uoto wa asili na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Discussion
Reader comments
0 contributions