Skip to main content

WANANCHI KISHIRI WAOMBA KUJENGEWA KITUO CHA POLISI

Wananchi wa Kata ya Kishiri, Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, wameomba kujengewa kituo cha polisi kutokana na kukua kwa eneo hilo na uhitaji mkubwa wa kuimarisha usalama wao na mali zao.

WANANCHI KISHIRI WAOMBA KUJENGEWA KITUO CHA POLISI

Wananchi wa Kata ya Kishiri, Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, wameomba kujengewa kituo cha polisi kutokana na kukua kwa eneo hilo na uhitaji mkubwa wa kuimarisha usalama wao na mali zao.

​Hayo yamejiri wakati wa mkutano wa hadhara wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, uliofanyika eneo la Kishiri Kati na wananchi wa kata hiyo.

"Kwa nini Kata ya Kishiri, ilivyokuwa kubwa kiasi hiki yenye idadi ya watu wengi, haina kituo cha polisi? Nina ushauri kwamba, RPC tunaomba tuboreshewe Kishiri yetu tuwe na kituo cha polisi," alisisitiza Juma Nkalango, mkazi wa Kishiri.

Mkutano huo ulikuwa ni mwendelezo wa kutoa elimu ya usalama kwa wananchi, kusikiliza kero za kiusalama na kuzitatua ili wananchi waendelee na shughuli zao za maendeleo kwa amani.

​"Hapa Kishiri tuna changamoto; changamoto ya kwanza, mji umekuwa, tunaomba tuwekewe kituo cha polisi," aliomba Manura Mafuru Antony.

Akizungumza katika mkutano huo, Kamanda Mutafungwa amesema kila mwananchi anawajibika kuzuia uhalifu katika eneo lake, na kwamba wajibu huo sio wa Jeshi la Polisi peke yake.

Amewataka kuwa wazalendo kwa kuipenda na kulinda nchi yao kwa kujiepusha na vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani, na mwisho amewataka kuishi kwa kufuata sheria za nchi.

​Kuhusu ombi la kujengewa kituo cha polisi, Kamanda Mutafungwa amemuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya na Mkuu wa Kituo cha Polisi Nyakato kukarabati Kituo cha Polisi Ndofe kilichokuwa kimeharibiwa kwa kuvunjwa vioo, na kuelekeza ifikapo Juni 22, 2026 kituo hicho kianze kutoa huduma kwa wananchi wa kata hiyo.

​Katika hatua nyingine, Kamanda Mutafungwa amewataka wananchi wa Kishiri kujitafakari na kujiepusha na vitendo vya kufanya uhalifu, ikiwemo kuharibu miundombinu ya Serikali.

​"Unakwenda kuchoma soko, ofisi ya Mtendaji wa Mtaa, unakwenda kupasua vioo vya kituo cha polisi, unakwenda kuharibu barabara kwa kuchoma matairi; kweli ni jambo zuri hilo?" alihoji Kamanda Mutafungwa.

​Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nyamagana, SSP Virginia Sodoka, ameshauri uongozi wa kata kupitia Mtendaji wa Kata hiyo, kukaa na kamati ya usalama ya kata ili kubainisha eneo ambalo watajenga kituo kikubwa cha polisi.

​"Mkishatafuta kiwanja, mtakuja Kituo cha Polisi Kati kuonana na mimi kwa ajili ya kupewa ramani na shughuli za ujenzi ziendelee,"

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.