Mbunge wa jimbo la Itwangi, Azza Hilal Hamad awahakikishia wakazi wa Nsalala upatikanaji wa maji safi Kufatia changamoto ya ukosefu wa upatikanaji wa maji safi na salama, katika kijiji Nsalala jimbo la Itwangi halimashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Azza mebainisha hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji hicho kwenye mkutano wa hadhara, ambapo kero yao kubwa ni kilio cha upatikanaji wa maji safi na salama.

Amesema, ajenda ya maji ni ya jimbo zima la Itwangi, na kwamba amekuwa wakilisemea Bungeni, na kuanisha kuwa wakati wakiendelea kusubili Maji ya Ziwa Victoria kufika katika kijiji hicho cha Nsalala, ameona ni vyema visima vya maji vya awali ambavyo viliharibika visafishwe na mashine na kuanza kuhudumia wananchi.
“Kisima kimoja kilichimbwa enzi za utawala wa marehemu Mzee Mwinyi na visima vyote viwili kimoja kilikuwa kinapeleka maji Nsalala na kingine Mwamkanga, nilisema haiwezekani ni kaa kusubiri mradi wa maji ya Ziwa Victoria na wakati tunavisima hapa,” amesema Azza.
Ameongeza kuwa, aliongea na Waziri wa Maji na Katibu Mkuu Wizara ya Maji wakatuma mashine ambazo zikafungua visima hivyo na vikakutwa visafi na maji yapo ya kutosha ambapo kisima cha kwanza kwa majibu ya wataalamu kinauwezo wa kutoa maji Lita 15,000 kwa saa moja na kingine Lita 10,000 kwa saa moja.
“Maji haya tuliyaonja hayana chumvi hata kidogo,” amesema Azza.

Ameongeza kuwa, baada ya Wataalamu kurudisha majibu kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji , alitoa ahadi kuwa haita fika Mwezi wa 12 Mwaka huu, wataleta pampu na kurudishia miundombinu ya mabomba na kuweka vituo vya kuchotea maji, wakati wakisubiri mradi wa Maji ya Ziwa Victoria.
Amezumgumzia pia barabara ya Nsalala- Butindi kwamba daraja lake lilivunjika muda mrefu, na kwamba ukifika Nela mvua za mwaka jana zilivunja karavati na pakawa hakuna mawasiliano, lakini Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ,kutokana na kwamba hataki wananchi wake wapate shida, ametoa fedha za ujenzi wa daraja hilo pamoja na karavati.
Katika hatua nyingine amezungumzia skimu ya umwagiliaji ya Nsalala na Skimu zingine kwamba ameshazisemea bungeni na kwamba serikali itakuja kutengeza mirefeji hiyo,huku akiwapongeza pia wananchi wa kijiji hicho cha Nsalala kwa kuanzisha ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho na kuamua kuwaunga mkono kwa kutoa shilingi milioni moja taslimu.

MASAKA KAMBESHA MENEJA HUDUMA KWA WATEJA SHUWASA
Kwa upande wake Meneja huduma kwa wateja SHUWASA, Masaka Kambesha, amesema Mamlala hiyo hua inamipango ya muda mrefu na mfupi na kwamba ya muda mfupi ndiyo hiyo ya ujenzi wa visima vya maji, na kwamba walifika Nsalala na kufanya usanifu na kuona uwezo na maji ya visima hivyo na kufika Desemba huduma ya kufufua visima hivyo itakuwa imeanza.
Amesema mpango wa muda mrefu ni kusambaza Maji ya Ziwa Victoria, na walishafanya usanifu na sasa wapo kwenye hatua nzuri ya kusambaza maji hayo katika vijiji kikiwamo cha Nsalala na sasa wanasubiri kupitishwa kwa andiko.
Nao baadhi ya wananchi wamempongeza Mbunge Azza kwa kuendelea kutatua changamoto ambazo zinawakabili wananchi hasa tatizo la maji.

Discussion
Reader comments
0 contributions