Wananchi takribani 500,000 wanatarajiwa kunufaika na Mradi wa Maji Kizimkazi, uliozinduliwa rasmi leo Agosti 13, 2026 na Rais Samia Suluhu Hassan.
Mradi huo, uliopo eneo la Pango la Machomwe, ni miongoni mwa miradi ya maendeleo inayozinduliwa katika shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi 2026.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kizimkazi, Naibu Waziri wa Maji na Nishati wa Zanzibar, Seif Kombo, amesema mradi huo utasaidia kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji katika eneo hilo.
Amesema chanzo hicho kinazalisha takribani lita milioni 2.4 za maji, wakati mahitaji ya eneo hilo ni takribani lita 500,000, hivyo kuwepo kwa ziada ya maji.

Seif amesema tenki lililojengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina uwezo wa kuhifadhi zaidi ya lita milioni moja, hatua inayotarajiwa kuimarisha upatikanaji wa maji kwa wananchi.

Discussion
Reader comments
0 contributions