Skip to main content

WANAHABARI NGUZO MUHIMU UFIKIAJI LENGO LA TAIFA MATUMIZI NISHATI SAFI YA KUPIKIA 2034

Na Eunice Kanumba - Morogoro.

WANAHABARI NGUZO MUHIMU UFIKIAJI LENGO LA TAIFA MATUMIZI NISHATI SAFI YA KUPIKIA 2034

Na Eunice Kanumba - Morogoro.

Wanahabari wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwa ni ajenda ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuchangia kufikiwa kwa lengo la Taifa la asilimia 80 ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Wito huo umetolewa  na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Habari Maelezo , Rodney Mbuya, wakati akifunga Warsha ya Kuwajengea Uwezo Waandishi wa Habari pamoja na Maafisa Mawasiliano wa Serikali kuhusu Uandishi na Uhamasishaji wa Masuala ya Nishati Safi ya Kupikia mkoani Morogoro.

Mbuya amesema, Serikali imeipa kipaumbele ajenda ya nishati safi ya kupikia kupitia Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa miaka 10 (2024–2034) na kwamba pamoja na mafanikio hayo, matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini yamefikia asilimia 28.6 ya kaya.

Hata hivyo, amesema bado kuna umuhimu wa kuongeza kasi ya utoaji wa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari ili kuhakikisha lengo la Taifa linafikiwa kwa wakati. Aidha, amesisitiza kuwa vyombo vya habari vya kitaifa na vya mikoani vina mchango mkubwa katika kuhamasisha jamii kubadili tabia na kukumbatia matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Aidha ameipongeza Wizara ya Nishati, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kupitia Mradi wa CookFund unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya pamoja na wadau wote wa nishati safi ya kupikia kwa kuandaa mafunzo hayo, akieleza kuwa yataongeza uwezo wa Waandishi wa Habari na Maafisa Mawasiliano wa Serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.