Skip to main content

WANAOTUHUMIWA KUCHOMA BWENI KENYA WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Takriban Wanafunzi tisa wanaotuhumiwa kupanga na kutekeleza shambulio la uchomaji moto katika shule ya Wasichana ya Utumishi iliyopo Nchini Kenya, lililosababisha vifo vya wasichana 16, wamefikishwa mahakamani hii leo Juni 2, 2026.

WANAOTUHUMIWA KUCHOMA BWENI KENYA WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Takriban Wanafunzi tisa wanaotuhumiwa kupanga na kutekeleza shambulio la uchomaji moto katika shule ya Wasichana ya Utumishi iliyopo Nchini Kenya, lililosababisha vifo vya wasichana 16, wamefikishwa mahakamani hii leo Juni 2, 2026.

Mbele ya Mahakama Kuu ya Mjini Naivasha, Mamlaka za uchunguzi ziliomba muda zaidi wa kuendelea wa kushugulikia tukio hilo na uamuzi utatolewa baadaye iwapo wasichana hao wataendelea kuzuiliwa kwa mwezi mmoja wakati uchunguzi ukiendelea.

Moto huo, uliozuka Mei 28 uliharibu bweni lililokuwa na Wanafunzi 202, ambapo uchunguzi, umeonesha msimamizi wa bweni alishindwa kufungua mlango wa dharura, hali iliyowalazimu wanafunzi wote kutoroka kupitia mlango mmoja pekee.

Hata hivyo, Wasichana wanaotuhumiwa wamekuwa chini ya ulinzi wa polisi kwa siku tano sasa na wakati wa mahojiano, ilibainika kuwa moto huo ulianzishwa kwa kuwasha godoro lililokuwa karibu na njia ya kutokea kwenye bweni kwa kutumia kiberiti na mafuta ya taa.

Matokeo ya vipimo vya DNA vinavyolenga kubaini utambulisho wa baadhi ya miili iliyoungua kiasi cha kutotambulika yanatarajiwa kutolewa kesho Jumatano Juni 3, 2026 huku sababu za tukio hilo zikiwa bado hazijulikani.

Picha za kamera za ulinzi (CCTV) zilizopatikana kutoka kwenye bweni lililoungua zinaonyesha wanafunzi sita wakiwasha moto huo, muda mfupi kabla ya wanafunzi wengine kuamka na kukimbia kujiokoa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.