Skip to main content

WANAFUNZI WALIOFARIKI KWA KUGONGWA NA LORI ARUMERU WAAGWA, DEREVA ASAKWA MIZIGO IKIZUIWA

Mizigo iliyokuwa imebebwa na lori lililosababisha ajali iliyoua Wanafunzi watatu wa Shule ya Sekondari Mringa wilayani Arumeru mkoani Arusha, imezuiwa hadi pale dereva wa lori hilo atakapopatikana.

WANAFUNZI WALIOFARIKI KWA KUGONGWA NA LORI ARUMERU WAAGWA, DEREVA ASAKWA MIZIGO IKIZUIWA
Studio Narration JAMBO FM

WANAFUNZI WALIOFARIKI KWA KUGONGWA NA LORI ARUMERU WAAGWA, D...

0:00 --:--

Mizigo iliyokuwa imebebwa na lori lililosababisha ajali iliyoua Wanafunzi watatu wa Shule ya Sekondari Mringa wilayani Arumeru mkoani Arusha, imezuiwa hadi pale dereva wa lori hilo atakapopatikana.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira amesema mizigo hiyo itabaki chini ya uangalizi wakati jitihada za kumpata dereva wa lori hilo zikiendelea.

Ajali hiyo, ilisababishwa na uzembe wa dereva wa lori aliyekuwa akipita magari mengine bila kuchukua tahadhari, ambapo lilicha njia na kugonga gari dogo lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara kabla ya kuwagonga wanafunzi hao watatu.

Wote walikuwa wakisoma kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Mringa, ambao wanaagwa hii leo Novemba 2, 2026, akiwemo Catherine Mussa anayetarajiwa kuzikwa Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Wengine ni Bianca Mgongo atazikwa Musoma mkoani Mara na6 Jesca Sabore Ng’otyek atazikwa Monduli mkoani Arusha.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.