Halmashauri ya Mji Babati imearifu uwepo wa jumla ya Wanafunzi 4,083 wanaofanya Mtihani wa Upimaji wa Taifa wa darasa la nne, wakiwemo Wavulana 2073 na Wasichana 2010.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, jumla ya Shule 49 za Halmashauri ya Mji hu9, zinashiriki Upimaji wa Taifa wa Darasa la Nne (SFNA).

Kati ya shule hizo, 35 ni za Serikali na 14 Binafsi, huku Shule 36 zikiwa ni za Mfumo wa Kiswahili, zikiwemo 35 za Serikali na 1 ya Binafsi na Shule 13 ni za mfumo wa Kiingereza zote ni Binafsi.
Mtihani wa Upimaji wa Taifa wa Darasa la Nne unafanyika kwa siku mbili za Oktoba 5-6, 2026.
Discussion
Reader comments
0 contributions