Jumla ya wanafunzi 3,007 wa Kidato cha Nne katika Manispaa ya Singida Mkoani Singida wanatarajiwa kuanza Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne utakaoanza leo Oktoba 19, 2026.
Idadi hiyo imebainishwa na Afisa Elimu, Elimu ya Watu Wazima na Mfumo Rasmi Idara ya Elimu Sekondari wa Manispaa ya Singida, Mwl. Siah Mtafya, wakati akizungumza na Jambo Media kuhusu maandalizi ya mtihani huo.
Mwalimu Mtafya amesema kati ya watahiniwa hao, wavulana ni 1,207 na wasichana ni 1,800, sawa na asilimia 75 ya wanafunzi waliojiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2023.
Afisa Elimu, Elimu ya Watu Wazima na Mfumo Rasmi Idara ya Elimu Sekondari wa Manispaa ya Singida, Mwl. Siah Mtafya.
Amebainisha kuwa jumla ya vituo vya mtihani ni 28, ambapo vituo 19 ni vya shule za Serikali na 9 ni vya shule binafsi.
Aidha, Mwl.Mtafya amewatakia kila la heri watahiniwa wote na kuwataka kumtanguliza Mungu katika kipindi chote cha mtihani.
Discussion
Reader comments
0 contributions