Skip to main content

WANAANGA WA ARTEMIS II WAREJEA DUNIANI SALAMA

Wanaanga wa Artemis II wamerejea salama Duniani wakihitimisha safari yao ya kihistoria ya siku tisa za dhamira yao ya kuuzunguka mwezi.

WANAANGA WA ARTEMIS II WAREJEA DUNIANI SALAMA

Wanaanga wa Artemis II wamerejea salama Duniani wakihitimisha safari yao ya kihistoria ya siku tisa za dhamira yao ya kuuzunguka mwezi.

Walitua katika Bahari ya Pasifiki majira ya saa 8:07 p.m. EDT (0007 UTC), huku kamanda Reid Wiseman akithibitisha kuwa Wanaanga wapo katika hali nzuri.

Wanaanga hao wanne, Reid (Kamanda wao), Victor, Christina na Jeremy walisafirishwa kwa Chopa kurudi kwenye meli ya jeshi la majini la Marekani kwa uchunguzi zaidi.

Kikosi cha Artemis II kilingia tena kwenye angahewa ya Dunia baada ya kukatika kwa mawasiliano kwa dakika sita, hali ambayo inadaiwa kuwa ni ya kawaida lakini yenye kutia wasiwasi.

Aprili 6, 2026, chombo hicho cha anga kilifikia umbali mkubwa zaidi kutoka Duniani wa Kilomita 406,771 (sawa na maili 252,756) wakati wa kupita karibu na Mwezi.

Hatua hii inavunja rekodi ya awali ya umbali mkubwa zaidi ambao binadamu wamewahi kusafiri angani na kuandika historia mpya.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.