Skip to main content

WALIOVAMIA ENEO LA MALISHO YA MIFUGO SERENGETI WATAKIWA KUONDOKA

Na Adam Msafiri - Mara.

WALIOVAMIA ENEO LA MALISHO YA MIFUGO SERENGETI WATAKIWA KUONDOKA
Studio Narration JAMBO FM

WALIOVAMIA ENEO LA MALISHO YA MIFUGO SERENGETI WATAKIWA KUON...

0:00 --:--

Na Adam Msafiri - Mara.

Serikali wilayani Serengeti mkoani Mara imetoa muda wa wiki mbili kwa wananchi waliovamia eneo la malisho ya mifugo linalomilikiwa na vijiji vya Kemgesi, Ring’wani na Masinki kuondoka mara moja, huku ikisisitiza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya viongozi waliohusika kuuza eneo hilo kinyume cha taratibu.

Akizungumza katika eneo hilo, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Angelina Marco amesema serikali haitavumilia uvamizi wa maeneo ya kijiji yaliyotengwa kwa matumizi ya pamoja ya wananchi, hususan shughuli za ufugaji.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Angelina Marco.

Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo, malisho hayo yametumika kwa zaidi ya miaka 50 na wananchi wa vijiji vya Kemgesi, Ring’wani na Masinki kwa shughuli za ufugaji wa mifugo. Hata hivyo, baadhi ya watu walivamia eneo hilo na kuanza shughuli za kilimo, makazi pamoja na ujenzi wa nyumba.

Wananchi wa vijiji hivyo wameeleza kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali wakisema zitaleta utulivu na kusaidia kulinda eneo hilo muhimu kwa wafugaji.

Baadhi ya wakazi wa Kemgesi, akiwemo Prosper Machage na Thom Mwita, wamesema uamuzi huo utasaidia kuondoa migogoro iliyokuwa ikiendelea katika eneo hilo na kurejesha matumizi halali ya ardhi ya malisho.

Kwa upande wao, viongozi wa vijiji wameahidi kushirikiana na serikali kuhakikisha eneo hilo linaendelea kulindwa dhidi ya uvamizi mwingine wowote.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kemgesi, Mwita Kebwe, amesema uongozi wa kijiji uko tayari kushirikiana na mamlaka zote husika ili kuhakikisha sheria na taratibu za matumizi ya ardhi zinazingatiwa.

Akizungumzia wananchi walionunua maeneo hayo, Mkuu wa Wilaya alisema serikali itaendelea kufuatilia malalamiko yao huku akisisitiza kuwa wale waliohusika kuuza maeneo hayo watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.