Skip to main content

WALIMU WENYE ULEMAVU KIGOMA WAOMBA UTATUZI WA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI

Walimu wenye ulemavu Mkoani Kigoma wameiomba Serikali kuchukua hatua za kutatua changamoto zinazowakabili katika mazingira yao ya kazi ili kuwawezesha utekelezaji wa majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

WALIMU WENYE ULEMAVU KIGOMA WAOMBA UTATUZI WA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI
Studio Narration JAMBO FM

WALIMU WENYE ULEMAVU KIGOMA WAOMBA UTATUZI WA CHANGAMOTO ZIN...

0:00 --:--

Walimu wenye ulemavu Mkoani Kigoma wameiomba Serikali kuchukua hatua za kutatua changamoto zinazowakabili katika mazingira yao ya kazi ili kuwawezesha utekelezaji wa majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Walimu hao walisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika mazingira ya kazi, hali ambayo wakati mwingine huathiri utekelezaji wa majukumu yao ya ufundishaji na utoaji wa huduma kwa wanafunzi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Kasulu, Mwalimu Elisha Kebelo, alisema chama hicho tayari kimepokea changamoto zinazowakabili walimu wenye ulemavu na kinaendelea kuzifanyia kazi kwa kushirikiana na mamlaka husika.

Mwenye wa Chama Cha Walimu Tanzania CWT wilaya ya Kasulu Mwl Elisha Kebelo, Picha na Tryphone Odace.

Aidha alisema kuwa uboreshaji wa mazingira kwa walimu wenye ulemavu unawasaidia kuweza kuendandana na mazingira na utoaji wa huduma kwa wanafunzi.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Kigoma, Mwalimu Cresensia Tindwa, alisema chama hicho kinaendelea kushirikiana na Serikali katika kutafuta suluhisho la changamoto hizo.

Alisema hatua hizo zinalenga kuhakikisha walimu wenye ulemavu wanapata mazingira rafiki ya kazi na wanawezeshwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa wakati.

Pichani ni miongoni mwa walimu wenye ulemavu wilayani Kasulu, Picha na Tryphone Odace.

Hata hivyo baadhi ya wadau mbalimbali wa elimu walisema kuwa ni muhimu kutambua mchango wa walimu katika maendeleo ya jamii na kujadili changamoto zinazohitaji kushughulikiwa ili kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.