Skip to main content

WALALAMIKA TANESCO KUHAMISHA NGUZO BILA TAARIFA KAHAMA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

WALALAMIKA TANESCO KUHAMISHA NGUZO BILA TAARIFA KAHAMA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

Wananchi wa Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, wamelalamikia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kwa kitendo cha kupeleka nguzo za umeme katika maeneo yao na baadaye kuziondoa hali wanayodai inachelewesha upatikanaji wa huduma hiyo muhimu.

Mkazi wa Kata ya Mhungula, Thimothy Chakupewa ameyasema haya kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika maegesho ya malori Kata ya Majengo, uliitishwa na Mbunge wa Jimbo la Kahama, Benjamini Ngaiwa kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.

Chakupewa amesema TANESCO imekuwa na tabia ya kupeleka nguzo za umeme katika maeneo yao na baadaye kuziondoa bila maelezo ya kuridhisha jambo linalozua maswali na malalamiko kwa wananchi wanaotarajia kupata huduma hiyo na inakatisha tamaa ya kupata umeme.

“Tuliletewa nguzo za umeme tukiamini tutapata huduma lakini baadaye zote zilibebwa na Tanesco na hadi sasa hatujapatiwa umeme. Tunaomba Mbunge uingilie kati ili kumaliza tatizo hili." Ameongeza Chakupewa.

Mkazi mwingine wa eneo la Mhongolo, Hawa Methord amesema wameomba huduma ya umeme muda mrefu bila mafanikio, licha ya kuwepo kwa nguzo zilizokwisha simikwa na nyingine bado zipo chini na kwamba hali hiyo inakatisha tamaa na kuwataka wahusika kuchukua hatua za haraka ili kila kaya ipate nishati ya umeme.

“Hii swala linachelewesha maendeleo kwa wakazi wa Kahama,nguzo wanazileta na kuzihamisha na hizi zingine zinachimbiwa na zinaachwa hivyohivyo,tunaomba wahusika wachukue hatua kwani wananchi tunahiaji huduma ya umeme sana,” amesema Bi Method.

Ofisa Mahusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Kahama, Robert Msemo akijibu malalamiko hayo amesema upatikanaji wa huduma hiyo unategemea uwepo wa rasilimali fedha na kwamba kwa sasa kuna mradi unaoendelea wa kusambaza umeme katika vitongoji husika.

“Sisi tunatoa huduma lakini hizi huduma zinategemea uwepo wa rasilimali fedha hivyo kwa sasa kuna mradi unaondelea wa kusambaza umeme katika vitongoji husika na niwahakikishie wananchi kuwa kila eneo tutafikisha huduma ya umeme,” amesema Msemo.

Amesema, wakati mwingine hulazimika kuondoa nguzo za umeme katika maeneo fulani na kuzipeleka kwenye maeneo yenye uhitaji wa dharura, kama yale yaliyopata uharibifu kutokana na ajali au shughuli za kibinadamu.

“Maeneo yote tuliyofikisha nguzo hatimaye hupatiwa huduma ya umeme. Tunafanya juhudi kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa kuhamisha nguzo baadhi ni sehemu ya kwenda kutatua tatizo ambapo limesababishwa na ajali au shughuli za kibinadamu," aliongeza Msemo.

Mbunge wa Jimbo la Kahama, Benjamini Ngaiwa amewataka TANESCO kuhakikisha wanatoa huduma kwa wakati na kuepuka tabia ya kupeleka nguzo na kuziondoa bila utekelezaji wa haraka wa huduma na kama kutakuwa na dharura basi wawajulishe wananchi kwanza.

Ngayiwa amesisitiza umuhimu wa kuwajibika kwa taasisi hiyo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya umeme kama ilivyopangwa na kuahidi kushirikiana na wabunge wa Msalala na Ushetu kuhakikisha fedha za maendeleo zinapatikana na wananchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.