Mkuu wa mkoa wa Shinyanga ametoa amewataka wakuu wa wilaya katika mkoa huo kwenda kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua pamoja na kusimamia miradi ya maendeleo ili gharama ya mradi iendane na thamnai ya mradi husika katika maeneo yao.

MKUU WA MKOA SHINYANGA MBONI MHITA
RC Mboni ametoa maagizo hayo leo tarehe 5 october 2026 katika hafla ya uapisho kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Dr Fransis Mlacha aliyeteuliwa hivi karibuni na rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan kuwa mkuu wa wilaya hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
RC Mboni amempongeza DC Mlacha kwa kuaminiwa na muheshimiwa rais kuwa mkuu wa wilaya ya Kahama huku akimtaka kulinda imani hiyo kwa kuafanya kazi kwa bidii na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) pamoja na dira ya taifa ya 2050.
Amesema utezi huo ukawe chachu kwa DC huyo katika suala zima la utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kuwahudumia wananchi na kutimiza azma ya serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na furaha.

Katika hatua nyingine RC Mhita amewataka wakurugenzi katika halimashauri zote sita za mkoa huo kuongeza makusanyo na mapato katika halimashuri zao ikiwa ni pamoja na kuzuia mianya ya upotevu wa mapato hayo kwani miradi mingi ya maendeleo katika halimashauri husika inategemea makusanyo ya mapato.
Aidha amewataka wakurugenzi hao kwenda kubuni vyanzo vipya vya mapato pamoja na kfanya utambuzi wa miradi ya maendeleo iliyosimama ili iweze kuendekea pamoja na kuongeza kasi ya ulipaji wa madeni katika halimashauri husika na kuhakikisha madeni hayaongeeki tena hususan kutokea kwa wazabuni.

PICHA YA PAMOJA YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA NA WAKURUGENZI KATIKA HALIMASHAURI ZA MKOA WA SHINYANGA
RC Mhita pia amewataka wakurugenzi kuendelea kusimamia suala la usafi katika mikondo na mifereje ya maji ikiwa ni hatua katika kuchukua tahadhari dhidi ya mvua za elnino zilizotabiriwa na mamlaka ya hewa Tanzania (TMA) ili kupunguza athari za mvua hizo zinazotarajiwa kunyesha juu ya wastani.

KUTOKA KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA KAHAMA DR FRANSIS MLACHA
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama Dr Fransis Mlacha mara baada ya kula kiapo amehaidi kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu katika kusimamia maendeleo ya wilaya ya Kahama kwa muongozo wa ilani ya chama cha mapinduzi 2025/2030 pamoja na dira ya taifa ya 2050.
Amesema anazifahamu changamoto za wilaya ya Khama kuwa ni pamoja na ubovu wa miundo mbinu ya barabara hivyo anakwenda kukabilian na changamoto hiyo ili wananchi wa Kahama wawee kufurahia serikali yao.
Dr Mlacha amesema anakwenda pia kusimamia suala zima la ukusanyaji mapato kwani kwa sasa Tanzania ipi katika mkakati wa kujitegemea hivyo pasipo makusanyo sahihi ya mapato yaitaipelekea nchi kujitegemea huku akighaidi kufanya kazi kwa unyenyekevu uadilifu na utii.

MKUU WA WILAYA YA KISHAPU PETER MASINDI
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa wilaya wenyeji mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi amesema maendeleo ya watu wa Kahama yanategemea utendaji kazi uliotukuka wa DC huyo na kmtaka kuendeleza miradi ya maendeleo iliyoachwa na watangulizi wake

Naye mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Shinyanga Mabara Mlolwa amemshukuru rais Samia kwa uteuzi huo kwani unakwenda kuongeza nguvu kazi na ari katika katika kutekeleza miradi ya maendeleo

Discussion
Reader comments
0 contributions