Na Afarah Suleiman, Babati - Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Mtatifikolo Kaganda na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Michael Semindu wamekutana katika kata ya magara sehemu ambayo Kuna mlima unaotenganisha Wilaya ya Babati na Wilaya ya Mbulu na kuona jinsi gani shughuli za kijamii zilivyoathiri mlima huo na kupelekea maporomoko katika baadhi ya maeneo ya kata ya magara.

Wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu kwenye mlima wa Mbulu, uliopo mpakani mwa Wilaya ya Mbulu na Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wametakiwa kuacha shughuli hizo mara moja, ili kuzuia wa uharibifu wa Maliasili, mabadiliko ya tabia ya nchi na kuharibu ziwa manyara kutoka na maporomoko ya kutoka milimani.

Hayo yamesemwa na Kamati za usalama za Babati na Mbulu, mara baada ya kwenda kujionea shughuli zinazoendelea katika mlima huo kinyume na utaratibu, ambazo ni Kilimo, Ufugaji na Uchimbaji wa Madini pia na makazi ya watu katika maeneo ya Mlima.



Discussion
Reader comments
0 contributions