Skip to main content

WAKUSANYA MAPATO SOKO LA SAMAKI NAMANGA WAINGIA 'RADA' ZA TAKUKURU KAHAMA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

WAKUSANYA MAPATO SOKO LA SAMAKI NAMANGA WAINGIA 'RADA' ZA TAKUKURU KAHAMA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

Serikali Wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), wilayani humo kuchunguza kikundi cha umoja wa wafanyabiashara wa Samaki Kahama (UWASAKA) kinachokusanya mapato ya Wafanyabiashara wa Samaki katika soko la Namanga Manispaa ya Kahama.

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika soko la namanga uliolenga kusikiliza na kutatua kero za wafanyabiashara wa soko hilo.

Nkinda ameigiza taasisi hiyo kuchunguza uhalali wa kikundi hicho kukusanya ushuru katika soko la Samaki licha ya kuwa wananchi wanalipa mapato yote ya serikali yanayotakiwa katika soko hilo.

‘Niwagize TAKUKURU chunguzeni kikundi hiki ambacho kinalalamikiwa na wafanyabiashara wa Samaki katika soko hili,baada ya kuchunguze mtuletee majibu ya uhalali wa wao kuhusika na mapato katika soko hili,” amesema Nkinda.

Katika hatua nyingine Nkinda ametoa wito kwa wafanyabiashara wote wanadaiwa mapato ya serikali kulipa fedha wanazodaiwa ili serikali iweze kutumia mapato hayo kuboresha miundombinu ya soko hilo ambayo ikiwemo barabara na majengo.

“Niwaombe sana wafanyabiashara ambao mnadaiwa mapato ya serikali,lipime mapato hayo ili serikali iweza kujenga miundombinu ya soko na kukarabati majengo ambayo yamechakaa,sasa kuna watu wanadaiwa toka mwaka 2021 hizo pesa ndizo zinazorudi kukarabati soko lenu sasa mtumie hizi siku mlizopewa na mkurugenzi wetu kulipa fedha hizo,” ameongeza Nkinda.

Awali wakizungumza katika mkutano huo baadhi ya wafanyabiashara wa Samaki ambao sio wanakikundi wa UWASAKA  wamesema kuwa wanalipa shilingi elfu nane kwa kila Kichwa kwenye kikundi hicho huku wakiilipa halmashauri shilingi Hamsini kwa kila kilo moja ya Samaki anayoingiza sokoni.

“Mh mkuu wa wilaya tunaomba kujua je kuna serikali ya manispaa ya Kahama na serikali ya hiki kikundi? Mana serikalini tunalipa mapato bado na kikundi hiki tunakilipa pesa ambazo hazifiki halmashauri watu wanagawana tunaomba mfuatilie swala hili ili tujue uhalali wa kikundi hiki cha watu wachache kukusanya mapato  kwa wafanyabiashara” wamesema wafanyabiashara hao.

Naye Mwenyekiti wa ujenzi wa soko Samaki Namanga Adam Jackson (Obama) amesema kuwa soko la Samaki Namanga walijenga kwa nguvu za kikundi cha UWASAKA kupitia mkopo wa benki na kwamba wafanyabiashara wanaolalamjika walikuja wenyewe kujiunga na wakakubaliana na Katiba ya kikundi hicho na kuiomba serikali kuwahamishia soko la majengo ikiwa wanaona tozo kubwa.

“ Hawa wenzetu hoja zao ziko sawa au pengine haziko sawa,sisi hapa tumejenga tena kwa mkopo na bado tunadaiwa na hawa wanaolalamika tuliwakaribisha wakakubaliana na Katiba yetu sasa tunashangaa wanalalamika,ushauri wetu wapelekwe kwenye soko la lilojengwa na serikali kule majengo” Amesema Jackson.

Mkuu wa wilaya ya Kahama, Frank Nkinda akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama amendelea kusikilliza na kutatua kero za wananchi katika maeeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kahama.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.