Wakufunzi Waelekezi na Wanafunzi wa Kozi ya Ukamanda na Unadhimu Kundi la 41/2026 wamefanya Ziara ya Kimafunzo mkoani Singida ikiwa na lengo la kujifunza kwa vitendo mchango wa maendeleo ya kiuchumi katika masuala ya ulinzi na usalama wa Taifa.
Ziara hiyo imefanyika Oktoba 12, 2026 na imeongozwa na Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania ambae pia ni Mkuu wa Msafara katikaziara hiyo, Meja Jenerali Stephen Justice Mnkande.
Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania Meja Jenerali Stephen Justice Mnkande.
Wakiwa Katika ziara hiyo, ujumbe umetembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Manispaa ya Singida na kiwanda cha Singida Fresh Oil Mills Ltd.
Katika maeneo yote yaliyotembelewa, ujumbe umepata fursa ya kupokea wasilisho juu ya mada isemayo "Economic Development for National Security"
Ziara ya kimafunzo ni sehemu muhimu ya mtaala wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu unaolenga kuwajengea uwezo Wakufunzi Waelekezi na Wanafunzi katika masuala ya uongozi wa kimkakati kwa kuona na kujifunza shughuli za maendeleo katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Discussion
Reader comments
0 contributions