Skip to main content

WAKOSOAJI WA SERIKALI WATEMBELEE KUJIONEA MAENDELEO YA MIRADI, MABORESHO YA HUDUMA - MAGANYA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Fadhili Maganya amemtaka Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche, na wanaharakati wengine wanaokosoa Serikali kutembelea maeneo mbalimbali nchini, ili kujionea maendeleo na maboresho ya huduma yanayoendelea.

WAKOSOAJI WA SERIKALI WATEMBELEE KUJIONEA MAENDELEO YA MIRADI, MABORESHO YA HUDUMA - MAGANYA
Studio Narration JAMBO FM

WAKOSOAJI WA SERIKALI WATEMBELEE KUJIONEA MAENDELEO YA MIRAD...

0:00 --:--

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Fadhili Maganya amemtaka Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche, na wanaharakati wengine wanaokosoa Serikali kutembelea maeneo mbalimbali nchini, ili kujionea maendeleo na maboresho ya huduma yanayoendelea.

Maganya amesema hayo leo wilayani Mbulu mkoani Manyara alipotembelea hospitali ya Wilaya kukagua jengo la Baba, mama na mtoto.

Amesema baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakidai Serikali haijafanya chochote, huku akiwataka wafike katika maeneo mbalimbali kuona ujenzi wa miundombinu, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na maboresho ya huduma kwa wananchi.

Amesema Tanzania ni nchi inayoendelea na maendeleo hayawezi kupatikana kwa wakati mmoja, hivyo ni muhimu kutambua hatua zilizofikiwa na kulinganisha huduma za sasa na hali ilivyokuwa miaka iliyopita.

“Tutawatengenezea ziara, watembee nchi hii hata kwa sampling baadhi ya mikoa tu, waone kazi kubwa ambayo imefanyika na inayoendelea kufanyika,” amesema Maganya.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.