Skip to main content

WAKAZI VIJIJI VYA JIRANI NA MPAKA HIFADHI YA SERENGETI WAIOMBA SERIKALI KUDHIBITI WANYAMA WAKALI, WAHARIBIFU

Na Adam Msafiri - Mara.

WAKAZI VIJIJI VYA JIRANI NA MPAKA HIFADHI YA SERENGETI WAIOMBA SERIKALI KUDHIBITI WANYAMA WAKALI, WAHARIBIFU

Na Adam Msafiri - Mara.

Baadhi ya wakazi wa vijiji vinavyopakana na mapori ya akiba ya Ikorongo na Grumeti wilayani Serengeti mkoani Mara, wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kudhibiti wanyama wakali na waharibifu wanaovamia makazi yao na kusababisha hofu pamoja na hasara za mara kwa mara.

Wananchi kutoka vijiji vya Nyanungu, Motukeri, Nyichoka na Tambiso wanasema wamekuwa wakiishi katika mazingira ya tahadhari kutokana na uwepo wa wanyamapori wanaoingia katika maeneo yao, hali inayohatarisha usalama wa watu na mali zao.

Wakizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, wananchi hao wameeleza kuwa pamoja na juhudi zinazofanywa na mamlaka husika, bado changamoto ya uvamizi wa wanyama inaendelea kuathiri maisha yao ya kila siku, hivyo wameomba kupatikana kwa suluhisho la kudumu litakalowalinda wao pamoja na shughuli zao za kiuchumi.

Akizungumza wakati wa ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Serengeti, Kanali Mtambi ameagiza kuanza mara moja kwa utekelezaji wa hatua za kudhibiti mwingiliano kati ya binadamu na wanyamapori, ikiwemo ujenzi wa uzio katika maeneo yanayoathirika zaidi.

Kwa upande wake, Afisa Mahusiano wa TAWA katika Mapori ya Akiba ya Grumeti na Ikorongo, Shija Alex, amesema taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na serikali pamoja na wananchi kuhakikisha hatua zinazochukuliwa zinasaidia kupunguza migogoro kati ya watu na wanyamapori.

Wananchi wa maeneo hayo wana matumaini kuwa utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa utasaidia kuimarisha usalama wao na kupunguza athari zinazotokana na uvamizi wa wanyama wakali na waharibifu katika vijiji vinavyozunguka mapori hayo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.