Faustine Kasala - Kigoma.
Wananchi wanaoishi katika vijiji vya mwambao mwa ziwa Tanganyika, kutoka Kata za Kagunga na Mwamgongo Wilaya ya Kigoma Mkoani Kigoma, wameiomba Serikali kupitia wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kukamilisha barabara ya Mkongoro hadi Kagunga yenye urefu wa kilometa 65, ili kufanikisha uwepo wa usafiri wa uhakika.
Kwa sasa wananchi, pamoja na watumishi wa umma, hulazimika kusafiri kwa kutumia mitubwi katika ziwa Tanganyika, kutokana na kukosa barabara ambayo ingefanikisha uwepo wa usafiri wa uhakika ambapo Wakazi wa kata za Kagunga na Mwamgongo wameomba serikali kukamilisha barabara iliyoanza kufunguliwa ili kuwa na uhakika wa usafiri.

Aidha Mkuu wa mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amekagua mradi wa kufungua barabara ya Mkongoro - Kagunga na kupokea taarifa kutoka kwa meneja TANROADS mkoa mhandis Elisony Mweladzi ambaye amebainisha kuwa, ujenzi wa barabara hiyo umesimama kutokana na ufinyu wa bajeti jambo ambalo Serikali inaendelea kulifanyia kazi.

Hata hivyo, RC Sirro amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua ili barabara hiyo ikamilike, huku akitoa wito kwa wakandarasi wanaokwamisha miradi kukamilika, kujitafakari na wale wanaoshindwa kumaliza kazi warudishe fedha za watanzania kabla ya sheria kufuata mkondo wake

Discussion
Reader comments
0 contributions