Skip to main content

WAKANDARASI WALIOPATA ZABUNI WATAMBULISHWA KWA RC DENDEGO

Na Saulo Stephen - Singida.

WAKANDARASI WALIOPATA ZABUNI WATAMBULISHWA KWA RC DENDEGO

Na Saulo Stephen - Singida.

Wakandarasi sita waliopata zabuni za utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa ofisi na makazi ya viongozi mkoani Singida, wametambulishwa rasmi kwa Mkuu wa Mkoa, Halima Dendego kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo. 

Utambulisho huo umefanyika katika kikao kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa wa Singida ikiwa ni kufuatia mikataba iliyosainiwa Aprili 24, 2026 kati ya Wakandarasi hao na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga, kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa miradi hiyo muhimu ya kiutawala.

Akizungumza katika kikao hicho, Rc Dendego amesisitiza utekelezaji wa kazi kwa viwango vya juu, akitaka miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kuzingatia thamani halisi ya fedha za umma ili kuleta tija kwa wananchi.

Aidha, amewaelekeza wakandarasi hao kufanya maboresho madogo yaliyoainishwa katika majengo ya Wilaya za Iramba, Manyoni na Singida, huku akisisitiza kuwa ofisi za Wakuu wa Wilaya zijengwe kuhamishiwa chini kwa kuzingatia miundombinu rafiki kwa wananchi wote, na urahisi wa upatikanaji wa huduma hususan watu wenye ulemavu.

Pamoja na hayo amehimiza wakandarasi kuhakikisha vijana wazawa wanapata ajira, hasa katika kazi zisizohitaji utaalamu mkubwa, ili kuongeza kipato na kushirikisha jamii moja kwa moja, akieleza kuwa miradi hiyo ni fursa ya kuongeza ujuzi kwa jamii ya Singida.

Kwa upande wao, wakandarasi waliotambulishwa wameahidi kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa na kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wa miradi hiyo, ikiwemo kutoa ajira kwa vijana wa Mkoa wa Singida wakati wa kipindi cha ujenzi.

Miradi hiyo inayogharamiwa kutoka Serikali Kuu, ni pamoja na ujenzi wa Ofisi za Wakuu wa Wilaya za Iramba, Manyoni na Singida, ujenzi wa makazi ya Wakuu wa Wilaya hizo, pamoja na ujenzi wa nyumba ya Katibu Tawala wa Mkoa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuimarisha uwajibikaji, kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza ufanisi katika utendaji wa serikali.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.