Skip to main content

WAJUMBE KAMATI YA LISHE SINGIDA WATAKIWA KUTEKELEZA MAAZIMIO KWA VITENDO

Na Saulo Stephen – Singida.

WAJUMBE KAMATI YA LISHE SINGIDA WATAKIWA KUTEKELEZA MAAZIMIO KWA VITENDO

Na Saulo Stephen – Singida.

Wajumbe wa Kamati ya Lishe Mkoa wa Singida wametakiwa kutekeleza kwa vitendo maazimio yaliyofikiwa katika Kikao cha Uhabarisho wa Muongozo wa Kamati ya Lishe na kuhakikisha wanawafikia walengwa wote katika jamii ili kuimarisha matumizi ya lishe bora.

Maelekezo hayo yametolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga, wakati akiongoza kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga.

Aidha, amesisitiza kuwa mafanikio ya utekelezaji wa afua za lishe yatategemea ushirikiano wa sekta zote, uwajibikaji wa kila mjumbe pamoja na ufuatiliaji wa karibu katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri.

Dkt. Mganga amesema kuna umuhimu wa kuimarisha afua za lishe hususan mashuleni, katika vituo vya afya na maeneo mengine muhimu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za lishe na hivyo kuboresha afya na ustawi wa jamii.

Katika kikao hicho, Afisa Lishe wa Mkoa wa Singida, Bi. Theda Sinde, aliwasilisha mada mbalimbali zilizolenga kuboresha hali ya lishe kwa makundi maalum ya wananchi. Miongoni mwa mada hizo ni huduma za lishe kwa watoto wenye umri wa miezi 0 hadi 23, hali ya lishe kwa wanaume, wanawake wajawazito pamoja na wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 49.

Baada ya majadiliano, wajumbe walikubaliana kuimarisha elimu ya afya na lishe kwa jamii ili kuongeza uelewa kuhusu ulaji bora na malezi sahihi ya watoto. Pia walisisitiza kuendelea kutoa elimu ya lishe kwa wanawake wajawazito, wanaonyonyesha na watoto, sambamba na kuimarisha huduma za ufuatiliaji wa ukuaji na maendeleo ya mtoto katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Jesca Lebba.

Aidha, kikao kiliazimia kuongeza ushiriki wa sekta mbalimbali katika utekelezaji wa afua za lishe na kuendeleza kampeni za kuhamasisha matumizi ya vyakula vyenye virutubishi vya kutosha ili kupunguza changamoto za utapiamlo na upungufu wa virutubishi katika jamii.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Jesca Lebba, ameahidi kuwa timu ya afya ya mkoa itaendelea kutoa ushirikiano na uwezeshaji wa kutosha kwa halmashauri zote ili kuhakikisha malengo ya kuboresha hali ya lishe katika Mkoa wa Singida yanafikiwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.