Skip to main content

WAJASIRIAMALI KATAVI WATUMIE TEKNOLOJIA KUFUNGUA MASOKO MAPYA - PINDA

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda, amewataka wajasiriamali wa Mkoa wa Katavi kutumia teknolojia na ubunifu kuongeza thamani ya bidhaa zao ili kufikia masoko mapya ndani na nje ya nchi.

WAJASIRIAMALI KATAVI WATUMIE TEKNOLOJIA KUFUNGUA MASOKO MAPYA - PINDA
Studio Narration JAMBO FM

WAJASIRIAMALI KATAVI WATUMIE TEKNOLOJIA KUFUNGUA MASOKO MAPY...

0:00 --:--

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda, amewataka wajasiriamali wa Mkoa wa Katavi kutumia teknolojia na ubunifu kuongeza thamani ya bidhaa zao ili kufikia masoko mapya ndani na nje ya nchi.

Mhe. Pinda ametoa wito huo Oktoba 29, 2026, alipokuwa akitembelea mabanda ya Halmashauri za Mkoa wa Katavi katika Maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi 2026 yanayoendelea katika Viwanja vya Mizengo Pinda, Kabungu, Wilaya ya Tanganyika.

Amesema maonesho hayo yanapaswa kutumiwa kama jukwaa la wajasiriamali kujifunza, kutangaza bidhaa zao na kutafuta masoko, huku akiwapongeza kwa ubunifu na hatua wanazochukua katika kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa mkoani humo.

Pinda amesema matumizi ya teknolojia ni muhimu katika kuboresha ubora wa bidhaa, kuongeza ushindani na kukidhi mahitaji ya soko, akiwataka wajasiriamali kuendana na mabadiliko ya teknolojia badala ya kutegemea masoko ya kawaida pekee.

“Nawapongeza wajasiriamali kwa ubunifu na ubora wa bidhaa zenu. Ni muhimu kuendelea kuboresha bidhaa hizo na kuendana na maendeleo ya teknolojia ili kuongeza ushindani na kupata masoko zaidi,” amesema Pinda.

Aidha, amewahimiza vijana kutumia ubunifu na fursa zilizopo kuanzisha biashara na kujiajiri, akieleza kuwa ujasiriamali unaweza kuwa kichocheo cha kuongeza kipato, ajira na maendeleo ya kiuchumi kwa Mkoa wa Katavi na Taifa kwa ujumla.

Maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi 2026 yanaendelea katika Viwanja vya Mizengo Pinda, Kabungu, yakiwa na kaulimbiu “Imarisha Uchumi Kutekeleza Dira ya Taifa 2050.”

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.