Na Eunice Kanumba – Shinyanga.
Vikundi vya wajasiriamali wadogo mkoani Shinyanga vinavyojishughulisha na usindikaji wa mazao nakuongeza mnyororo wa thamani vimeishukuru serikali mkoani Shinyanga kuwapa fursa ya kushiriki maonyesho ya kimataifa ya biashara ya hamsini maarufu kama maonyesho ya saba saba yanayotarajiwa kuanza mwanazoni mwa mwezi Julai 2026.
Wakizungumza na jambo media kuhusiana na fursa hizo baadhi ya wafanyabiashara waliopata firsa hiyo wakiwemo wachimbaji wadogo pamoja na wanawake na vijana waliopatiwa mikopo ya asilimia kumi na halimashauri za mkoa wa mkoa wa Shinyanga wamesema wameishukuru serukali kwa fursa hiyo na kwamba linakwenda kuwa jukwaa muhimu kwao katika kujifunza kwa wafanyabiashara wengine na kubadilishana uzoefu.

Joseph Lukas ni mfanyabishara wa nguo za mitumba katika soko la Ngokolo manispaa ya Shinyanga hakusita kuelezea furaha yake kwa jambo media juu ya fursa hiyo na kwamba itamuongezea uzoefu wa namna ya kufanya biashara kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa katika maonyesho hayo na kuweza kujua taratiu rasimi za mifumo mbalimbali ya kibiashara.
“Fursa hii kwetu ni muhimu sana kwasababu na sisi tunaitaji kukua kibiashara kwa hiyo tunaishukuru serikali ya mkoa na tunahaidi kwenda kujifunza Zaidi ili kukuza mitaji yetu kwani tutakwenda kukutana na wafanyabiashara wengi kutoka katika mataifa mbalimbali,“ amesema Lukas.

Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akitoa taarifa ya ushiriki wa mkoa huo katika maonyesho ya hamsini ya sabasaba amesema hii ni awamu ya pili kwa mkoa huo kushiriki kwa mara ya kwanza mkoa huo ulishiriki mwaka 2025 kwa mafanikio makubwa yaliyoleta matokeo chanya kwa wafanyabiashara katika mkoa huo.
“Maonesho ya Sabasaba yameendelea kuwa moja ya jukwaa kubwa la kibiashara nchini Tanzania, yakitoa fursa kwa wazalishaji na wafanyabiashara kujitangaza, kujifunza na kupanua mitandao ya kibiashara katika soko la kimataifa,” alisema RC Mhita.

Maonyesho ya biashara ya sabasaba ni jukwaa muhimu linalowakutanisha wafanyabiashara, wawekezaji, wazalishaji na watoa huduma kutoka Tanzania na mataifa mbalimbali duniani, Kupitia usimamizi wa TANTRADE, maonesho hayo yameendelea kukuza biashara, kuhamasisha uwekezaji na kutoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa kuonesha bidhaa na huduma zao kwa umma.
Discussion
Reader comments
0 contributions