Skip to main content

WAISLAMU TUEPUKE URAIBU WA GADHABU - SHEIKH SWEDI

Na Gideon Gregory - Dodoma.

WAISLAMU TUEPUKE URAIBU WA GADHABU - SHEIKH SWEDI

Na Gideon Gregory - Dodoma.

Katibu wa Sekretarieti ya Baraza la Ulamaa Taifa na Mratibu wa Ofisi ya Mufti Tanzania, Sheikh Swedi Twaibu Swedi, amewasihi waumini wa Kiislamu kujiepusha na tabia ya kuwa waraibu wa ghadhabu (hasira) pamoja na matumizi mabaya ya teknolojia, akisema mambo hayo mawili yamekuwa chanzo cha migogoro, kuvunjika kwa maadili na kuharibika kwa mahusiano katika jamii.

Akizungumza katika Msikiti wa Masjid Ghazali jijini Dodoma wakati wa kutoa mawaidha kwa waumini, Sheikh Swedi amesema kuwa maendeleo ya teknolojia yameleta manufaa makubwa katika maisha ya binadamu, lakini pia yameambatana na changamoto kutokana na baadhi ya watu kuitumia bila elimu na maarifa sahihi.

Amesema kuwa mitandao ya kijamii kama TikTok, Instagram na majukwaa mengine imekuwa sehemu ambayo watu wengi hujikuta wakifanya makosa kutokana na kushindwa kudhibiti hasira zao, hali inayosababisha kutukana, kudhalilishana na kusambaza taarifa bila kufanya uchunguzi wa ukweli wake.

"Kuna jambo linalotusumbua sana katika zama hizi, nalo ni teknolojia. Tatizo si teknolojia yenyewe, bali namna tulivyoipokea na kuitumia. Ilipopita mikononi mwetu na kwenye viganja vyetu kupitia smartphones na computers, baadhi ya watu wameitumia vibaya kwa sababu ya kukosa maarifa ya kuitumia kwa usahihi," amesema.

Aidha, amesitiza kuwa mtu ambaye hana uelewa wa matumizi sahihi ya teknolojia anaweza kupokea message, kuifanya forward au kuandika comment bila kufikiria athari zake, jambo ambalo linaweza kusababisha madhara makubwa duniani na Akhera.

Sheikh Swedi amewakumbusha waumini kuwa Mwenyezi Mungu amewataka waumini kuthibitisha habari kabla ya kuzieneza. Alinukuu mafundisho ya Qur'ani yanayowaelekeza waumini kufanya uchunguzi wa habari wanazozipokea ili kuepusha kuwatendea watu dhuluma kutokana na taarifa zisizo za kweli.

Amesema katika zama za sasa watu wengi hawaonani ana kwa ana bali hukutana kupitia smartphones na mitandao ya kijamii, hivyo ni muhimu kutumia busara katika kuandika comments, kujibu messages na kushirikisha taarifa kwa uwajibikaji ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima.

Akizungumzia ghadhabu, Sheikh Swedi amesema hasira ni miongoni mwa mambo ambayo Mtume Muhammad (S.A.W.) aliwahimiza Waislamu wajiepushe nayo kwa kuwa humfanya mtu kushindwa kufikiri kwa busara na kuchukua maamuzi yanayoweza kumletea majuto.

Ameeleza kuwa kwa mujibu wa wataalamu wa sayansi, hasira huambatana na mabadiliko ya kemikali mwilini yanayoweza kumfanya mtu ashindwe kujitawala, jambo linaloweza kumpelekea kufanya vitendo vya ukatili, matusi au maamuzi ya haraka yasiyo sahihi.

"Hasira huja pale mtu anapoudhiwa, anapodhulumiwa au anapokasirishwa. Lakini Uislamu unatufundisha kujizuia na kuitawala nafsi yetu badala ya kutawaliwa na hasira," amesema.

Amefafanua kuwa teknolojia ya kisasa ni mkusanyiko wa mbinu, vifaa na maarifa yanayolenga kurahisisha maisha ya binadamu na kutatua changamoto mbalimbali. Hata hivyo, alisema teknolojia hiyo inapogeuzwa kuwa chombo cha matusi, uchochezi, uongo na udhalilishaji, hupoteza lengo lake halisi.

Sheikh Swedi amewataka waumini kutumia smartphones, computers na mitandao ya kijamii kwa ajili ya kujifunza, kuelimishana, kueneza maadili mema na kuimarisha mshikamano wa jamii badala ya kuzitumia kueneza chuki na migogoro

Pia, amewasihi waumini kujenga tabia ya kujitafakari kabla ya kuandika, kurekodi au kusambaza jambo lolote kwenye mitandao ya kijamii wakikumbuka kuwa kila neno na kitendo chao kitawajibishwa mbele ya Mwenyezi Mungu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.