Skip to main content

WAHITIMU VYUO VIKUU WASHAURIWA KUTAZAMA FUSRA MAFUNZO YA UFUNDI STADI

Na Saulo Stephen - Singida.

WAHITIMU VYUO VIKUU WASHAURIWA KUTAZAMA FUSRA MAFUNZO YA UFUNDI STADI

Na Saulo Stephen - Singida.

Wahitimu wa vyuo vikuu nchini wametakiwa kutazama fursa za mafunzo ya ufundi stadi kama njia mbadala ya kukabiliana na ushindani katika soko la ajira, kwa kujifunza fani mbalimbali zitakazowawezesha kujiajiri na kuanzisha shughuli za uzalishaji.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Chuo cha VETA Mkoa wa Singida, Mkufunzi Mathias Pastory, wakati akizungumza na Jambo Media, ambapo amesisitiza umuhimu kwa vijana kubadili mtazamo wa kusubiri ajira za kuajiriwa na badala yake kujenga uwezo wa kujiajiri kupitia ujuzi wa vitendo.

Mkuu wa Chuo cha VETA Mkoani Singida, Mkufunzi Mathias Pastory.

Pastory amesema elimu ya chuo kikuu inaweza kuongezewa thamani kwa kupata ujuzi wa ufundi unaoweza kutumika moja kwa moja katika uzalishaji, akitaja fani mbalimbali zinazoweza kuwa chanzo cha ajira na kipato kwa vijana.

“Vijana wasione kwamba kumaliza chuo kikuu ndio mwisho wa kujifunza. Wanaweza kuja VETA wakajifunza fani mbalimbali ambazo zitawasaidia kujiajiri, kuanzisha biashara na kujikwamua kiuchumi,” amesema Pastory.

Amesema mabadiliko katika soko la ajira yanahitaji vijana kuwa na ujuzi unaoweza kutatua changamoto za jamii, badala ya kutegemea nafasi chache za ajira rasmi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.