Skip to main content

WAHITIMU MAFUNZO YA UFUGAJI SAMAKI, UCHAKATAJI KIGOMA WAASWA KUYATUMIA KWA WELEDI

Na Faustine Kasala - Kigoma.

WAHITIMU MAFUNZO YA UFUGAJI SAMAKI, UCHAKATAJI KIGOMA WAASWA KUYATUMIA KWA WELEDI

Na Faustine Kasala - Kigoma.

Zaidi ya vijana 40 kutoka wilaya tatu za Mkoa wa Kigoma, Kasulu, Kibondo na Buhigwe, wamehitimu mafunzo ya ufugaji wa samaki na uchakataji wa mazao ya samaki yaliyotolewa na Chuo cha FETA Mkoani Kigoma ambayo yatawasaidia kuinua uchumi wao na hata kuchangia maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika katika Chuo cha Mati Mubondo Halmashauri ya Mji Kasulu, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Tanzania, Dkt. Semvua Mzighani, amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kuongeza ujuzi kwa vijana na kuwajengea uwezo wa kujiajiri.

"Ninaimani vijana mpo katika vita kubwa ya kujipambania kimaisha, mnatafuta kila njia ili mtimize ndoto zenu, na hii ndio njia sahihi itakayowasaidia kutimiza ndoto zenu, kuongeza ujuzi na maarifa, tumieni maarifa haya kuwafundisha na wengine ambao hawakupata fursa ya kushiriki, naamini hatua hii itawasaidia kuongeza uzalishaji wa samaki, kuimarisha usalama wa chakula na kuinua uchumi wa familia na taifa kwa ujumla," alisema Dkt. Mzighani.

Naye Mkuu wa Chuo cha FETA Tawi la Kigoma, August Shirima, amesema mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha vijana kujiari na kupata ujuzi wa kisasa wa ufugaji wa samaki na uchakataji wa mazao yake ili waweze kuanzisha shughuli za uzalishaji zenye tija na kujiongezea kipato.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema yatawasaidia kuongeza maarifa mapya ya kuanzisha miradi ya ufugaji wa samaki na uchakataji wa mazao yake jambo ambalo litawafanya kutekeleza shughuli za ufugaji na uchakataji wa mazao ya Samaki kwa kujiamini

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.