Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Upendo Wella, amewataka wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kutumia maarifa, ujuzi na uzoefu walioupata kambini kwa manufaa ya familia, jamii na taifa.
DC Wella ameyasema hayo jana 08/09/2026 wakati wa mahafali ya vikosi viwili vya JKT yaliyofanyika katika Kambi ya Msange, Tabora, ambapo amesisitiza umuhimu wa vijana kutumia mafunzo hayo katika kujenga maisha yenye nidhamu, uwajibikaji na kujitegemea.

Mafunzo ya JKT yameelezwa kuwa ni nyenzo muhimu katika kuwajenga vijana wenye nidhamu, uzalendo, ukakamavu na ujuzi wa kujitegemea, huku baadhi ya wahitimu wakieleza kuwa hofu waliyokuwa nayo kabla ya kuingia kambini imegeuka kuwa fursa muhimu ya kubadilisha mtazamo wao kuhusu maisha.
Aidha, Mkuu wa Mafunzo wa JKT, Brigedia Generali Peter Mnyani, amewataka wahitimu kutumia ipasavyo ujuzi walioupata na kuwa mfano bora katika familia, jamii na taifa.

Wahitimu hao pia wamewahimiza vijana wenzao kutokuwa na hofu ya kujiunga na JKT, wakieleza kuwa mafunzo hayo yamekuwa na manufaa makubwa katika maisha yao, hususan katika kujenga nidhamu, kujiamini na kuwajibika.




Discussion
Reader comments
0 contributions