Skip to main content

WAHIMIZWA KUPINGA UKATILI, NDOA ZA UTOTONI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limetoa elimu kwa wanawake wa Kata ya Mahembe, Wilaya ya Kigoma kuhusu kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto.

WAHIMIZWA KUPINGA UKATILI, NDOA ZA UTOTONI
Studio Narration JAMBO FM

WAHIMIZWA KUPINGA UKATILI, NDOA ZA UTOTONI

0:00 --:--

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limetoa elimu kwa wanawake wa Kata ya Mahembe, Wilaya ya Kigoma kuhusu kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto.

Akitoa elimu hiyo Oktoba 31, 2026 Mkaguzi wa Polisi, Anna Daudi amewataka wanawake hao kutokuwa sehemu ya kuficha vitendo vya ukatili na unyanyasaji, bali wawe mstari wa mbele kuripoti vitendo hivyo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.

Insp. Daudi amesisitiza umuhimu wa jamii kushirikiana katika kuzuia mimba na ndoa za utotoni, hususan kwa watoto wa kike, akieleza kuwa jamii ina wajibu wa kuwalinda watoto na kuhakikisha wanapata haki zao za msingi.

Vile vile INSP Anna amewataka wanawake kutambua nafasi na wajibu wao katika kudumisha amani na usalama wa jamii kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na kutoa taarifa mapema kuhusu viashiria vya uhalifu katika maeneo yao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.