Skip to main content

WAHANGA JANGA LA MOTO KAHAMA WAIOMBA SERIKALI IWASHIKE MKONO

Wajasiliamali wadogo wanaofanya shughuli zao katika eneo la viwanda Zongomela maarufu Dodoma Wilayani Kahama mkoan Shinyanga, ambao ofisi zao ziliteketea kwa moto hivi karibuni, wameiomba serikali kuwashika mkono kwa kuwapatia mikopo, ili wanunue mashine na kujenga mabanda yao ili wajikwamue kiuchumi.

WAHANGA JANGA LA MOTO KAHAMA WAIOMBA SERIKALI IWASHIKE MKONO

Wajasiliamali wadogo wanaofanya shughuli zao katika eneo la viwanda Zongomela maarufu Dodoma Wilayani Kahama mkoan Shinyanga, ambao ofisi zao ziliteketea kwa moto hivi karibuni, wameiomba serikali kuwashika mkono kwa kuwapatia mikopo, ili wanunue mashine na kujenga mabanda yao ili wajikwamue kiuchumi.

Wakiongea na waandishi wa habari katika kikao chao kilicholenga kujadili namna ya kupata mitaji mipya wajasiliamali hao wamesema kuwa kwa sasa hawana mitaji yoyote kutokana na mashine zao kuteketea Pamoja na mbao za Samani malimbali za wateja hali inayowafanya washindwe kulipa kodi za serikali na kuendesha familia zao.

“Sisi ombi letu kwa serikali tunaomba watusaidie mikopo hata ile ya watu watano watano ili itusaidie kurejesha mitaji yetu kwakuwa hatuna kabisa mitaji hali inayotufanya tushindwe kulipa kodi za serikali na kushindwa kuendesha maisha yetu sisi na familia zetu” Wamesema wajasiliamali hao.

Sambamba na hayo wamemuomba Mbunge wa jimbo la Kahama mjini Benjamini Ngayiwa kuwasaidia kupata mikopo hiyo hata kwa kujiunga vikundi vya watu watano watano kwani wanaweza kujisimamia na kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa kwa wakati.

“Tunamuomba Mbunge wetu Mh Ngayiwa atusaidie kupata hii mikopo kwani alikuja eneo hili na akajionea hali ilivyokuwa katika maeneo yetu,hivyo tunamuomba atupiganie sisi wajasiliamali ambao tumepata janga la moto na mali zetu kuteketea,” wameongeza wajasiliamali hao.

Katika hatua nyingine wameomba uongozi wa soko kuwasaidia fedha zilizochangishwa na wafanyabiashara wengine kama mkono wa pole ili ziwasaidie kununua vitu vidogo vidogo ambavyo vimeharibiwa na janga la moto kwani umepita muda mrefu fedha hizo hawajapewa na hawajui zipo kwa nani.

“Tunaomba sana Mwenyekiti wa kiwanda chetu atusaidie fedha ambazo wafanyabiashara wenzetu wamechanga kwa ajili ya watu walionguliwa na mali zao, fedha hizi japo ni kidogo nina Imani zinaweza kutusaidia hata kununua mabati chakavu,kwa maana hadi leo hatujua fedha hizo ni shilingi ngapi na zipo wapi sasa tunaomba uongozi utusaidie katika hili” Wameongeza Wajasiliamali hao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa eneo la viwanda Dodoma Tembo Rashid amesema kuwa uongozi wa eneo la viwanda uliweka mkakati wa kukusanya fedha kwa ajili ya kuwasaidia wahanga hao na kwamba zoezi hilo litakamilika wiki hii na wanatarajia kuwapa fedha siku ya ijumaa.

“Sisi kama uongozi tuliweka mkakati wa kukusanya fedha kwa ajili ya kuwasaidia wenzetu kiasi kidogo cha fedha na matumaini yetu siku ya ijumaa tutawapatia fedha hizo,lakini tunaiomba serikali kupitia mfuko wa maafa itasaidie katika hili mana wanakuja hapa na kukusanya kodi na sisi tunatoa fedha serikalini.” Amesema Rashid.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, Jumla ya wajasiliamali thelathini na sita katika eneo la viwanda Zongomela walifikwa na janga la moto kwa kuunguliwa vitendea kazi vyao zikiwemo mashine na malighafi mbalimbali za wateja na kwamba hii ni mara ya tatu kwa eneo hilo kuungua moto.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.