Idara ya uhamiaji Mkoani Kigoma imefanikiwa kuwakamata wahamiaji 4495 kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba huku wengine 1258 wakikamatwa mwezi Octoba kupitia operesheni na misako mbalimbali ilifanyika katika maeneo yote ya Mkoa wa Kigoma.
Hayo yamebainishwa na Afisa uhamiaji Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Dismas Mlula wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo amesema mpaka sasa wahamiaji haramu 4350 wamerudishwa nchi mwao.
Amesema kuwa wengi wa waliokamatwa waliingia kinyume cha sheria na hawakuwa na nyaraka zinazowaruhusu kuishi nchini huku raia wa Burundi wakiwa wengi zaidi.

Afisa uhamiaji Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Dismas Mlula, Pcha na Tryphone Odace
Mlula amesema Mkoa wa Kigoma wahamiaji haramu wanakuwa wengi kwa kuwa ndio lango la kuingilia na kuelekea mikoa mingine huku shughuli za kilimo zikiwa ni miongoni mwa sababu ya wengi wao kuja nchi.
Aidha amewataka viongozi wa serikali za mitaa na vijiji kuendelea kushirikiana na wananchi katika kudhibiti uingiaji holela wa watu ambao sio raia wa Tanzania ili kuhakikisha wimbi la wahamiaji haramu linapungua na kuwa wataendelea kutoa elimu kupitia kupitia kampeni ya mjue jirani yako ili kuhakikisha wananchi wanatambua namna ya kuwatambua wahamiaji haramu.
Aidha, amewataka viongozi wa serikali za mitaa na vijiji kuendelea kushirikiana na wananchi katika kudhibiti uingiaji holela wa watu wasiokuwa raia wa Tanzania, akisisitiza kuwa ushirikiano huo utasaidia kupunguza wahamiaji wanaoingia nchini kinyume cha sheria.

Baadhi ya wahamiaji haramu waliokamatwa, Picha na Ofisa habari Uhamiaji Kigoma
Amesema Idara ya Uhamiaji itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia kampeni ya “Mjue Jirani Yako” ili kuwajengea uelewa wa namna ya kutambua na kutoa taarifa kuhusu wahamiaji wanaoishi nchini bila kufuata taratibu za kisheria.
Hata hivyo wananchi Mkoani Kigoma akiwemo Richard Michael na Jackson Mshobozi wameiomba serikali kuitia idara ya uhamiaji Mkoa kuhakikisha wanaendelea kufanya operesheni ili kubaini wahamiaji haramu na kuwachukulia hatua wanaowaficha wahamiaji haramu
Discussion
Reader comments
0 contributions