Skip to main content

WAFANYABIASHARA MIRERANI WAWASILISHA KERO, WAOMBA MABORESHO SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MADINI

Na Afarah Suleiman, Mirerani - Manyara.

WAFANYABIASHARA MIRERANI WAWASILISHA KERO, WAOMBA MABORESHO  SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MADINI
Studio Narration JAMBO FM

WAFANYABIASHARA MIRERANI WAWASILISHA KERO, WAOMBA MABORESHO...

0:00 --:--

Na Afarah Suleiman, Mirerani - Manyara.

Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini ya Tanzanite wa Mirerani, Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara, wamewasilisha changamoto kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Fadhili Maganya, wakiitaka Serikali kuzitafutia ufumbuzi, ili kuboresha mazingira ya uchimbaji na biashara ya madini hayo.

Changamoto hizo ni gharama kubwa za umeme, hasa malipo ya KVA; gharama za vilipuzi; upatikanaji wa mitaji kwa wachimbaji wa madini ya vito, hususan Tanzanite na Green Garnet; pamoja na changamoto ya masoko ya Tanzanite, huku wakitaka Serikali kusaidia kuitangaza zaidi kimataifa.

Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara (MAREMA), Elisha Mnyawi, amesema kupunguza gharama za uzalishaji na kuwawezesha wachimbaji kupata mitaji kutasaidia kuongeza uzalishaji na mapato ya Serikali.

Amesema Tanzanite inahitaji kutangazwa zaidi katika masoko ya kimataifa, akitaja maonesho ya madini katika China, Japan, Thailand na Tucson nchini Marekani kuwa miongoni mwa maeneo ambayo Tanzania inaweza kutumia kutafuta masoko mapya.

Akijibu changamoto hizo, Maganya amesema amefika Mirerani mahsusi kusikiliza wafanyabiashara na wachimbaji wa Tanzanite na atachukua hoja zao kuzifikisha kwa viongozi na mamlaka zinazohusika.

Amesema Tanzanite imebeba maisha ya Watanzania wengi, hivyo changamoto zinazohusu sekta hiyo hazipaswi kupuuzwa, bali zinahitaji kusikilizwa na kutafutiwa majibu.

Maganya amesema nafasi yake ni kusikiliza wananchi na wadau katika maeneo mbalimbali na kuwasilisha hoja zao sehemu husika, akisisitiza kuwa CCM ina wajibu wa kusikiliza makundi yanayofanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Amesema alihakikisha Mirerani haiondolewi katika ratiba ya ziara yake ili apate fursa ya kukutana na wafanyabiashara wa Tanzanite na kusikia moja kwa moja hali wanayokutana nayo.

“Niliwaambia pangeni popote, futeni popote, punguzeni popote, lakini Mirerani msipunguze nikutane na wafanyabiashara wa Tanzanite,” amesema.

Maganya amesema changamoto zinapowasilishwa na wananchi, jambo la msingi ni kuzitafuta majawabu, na pale inapobainika kuwa sheria au taratibu zinahitaji maboresho, suala hilo linaweza kuwasilishwa kwa mamlaka husika.

Amesema atawasilisha hoja za wachimbaji na wafanyabiashara wa Mirerani ili ziweze kufanyiwa kazi, huku akiwataka wadau hao kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza sekta ya madini.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.