Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Jackson Kiswaga imejadili namna ya kuimarisha ushirikishwaji wa wadau katika utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji, katika kikao kilichofanyika Oktoba 19, 2026.
Akiwasilisha mada kwa niaba ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Robert Sunday, ameeleza mchango wa Bodi za Maji za Mabonde na wadau mbalimbali katika kulinda rasilimali hiyo muhimu.

Hata hivyo, Wajumbe wa Kamati wameipongeza Wizara ya Maji kwa juhudi zake na kutoa mapendekezo ya kuimarisha ushirikishwaji wa wadau, kwa lengo la kuhakikisha vyanzo vya maji vinahifadhiwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Discussion
Reader comments
0 contributions